Tuesday, December 3, 2013

KINANA AENDELEA NA ZIARA KATIKA JIMBO LA MBEYA VIJIJINI

1 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa msingi wa Zahanati katika kijiji cha Chamwengo Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya vijijini wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo na utekelezaji wa ilani ya uchagzui ya CCM katika ziara yake ya wilaya ya mbeya vijijini, Katika ziara hiyo Kinana anafuatana na wajumbe wa halmashauri kuu taifa Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC itikadi na uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC siasa na Uhusiano wa kimataifa na leo anaendelea na ziara hiyo Jimbo la Mbeya Vijijini kabla ya kumalizia kesho ambapo anatarajia kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe mjini Mbeya  2 

Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akishiriki ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Chamwengo kata ya Inyala leo. 3 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigala wakiwa katika ujenzi wa zahanati hiyo leo. 4 
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigala  akiliweka sawa tofari wakati akishiriki ujenzi wa zahatati katika kijiji cha Chamwengo kata ya Inyala leo. 5 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua tanki la maji linalojengwa katika kijiji cha Itimu kata ya Iwindi Mbeya vjijini. 6 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza na mjumbe mmoja wa mabalozi wakati alipokuwa akielekea kufungua shina la CCM mjini Mbalizi 8 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana  akikabidhi kadi kwa mmoja wa wanachama waliojiunga na chama hicho wakati alipofungua moja ya matawi ya chama hicho mjini Mbalizi 9 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wananchama waliojiunga katika tawi hilo 11 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake pamoja na viongozi wenzake wakielekea kwenye mkutano wa ndani.
Post a Comment