Wednesday, December 11, 2013

WASANII wa maigizo na ngoma za asili wametakiwa kuacha tabia ya kuiga tamaduni za nchi za nje na kuzifanyia kazi badala ya kuenzi utamaduni wa Nchi yao kupitia sanaa wanazizifanya.


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Norman Sigalla ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, wakati wa uzinduzi wa Chama cha Sanaa Jiji la Mbeya(CHASAMBE) uliofanyika katika Viwanja vya chuo cha Uhasibu (TIA) Jijini hapa.
Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga akiongea na wasanii hao
 Mwenyekiti wa Chama cha sanaa jiji la Mbeya  Samweli Mwamboma alisema madhumuni ya kuanzisha chama na kukizindua rasmi ni kutetea maslahi ya wasanii wa sanaa zote.
Baadhi ya Wasanii wa jiji la Mbeya  wakijiandaa kwenda kutoa msaada kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya wazazi ya Meta wakati wa uzinduzi wa chama chao.
Kaimu katibu Mkuu wa Chama cha sanaa Jiji la Mbeya, Bahati Shulula akimjulia hali mmoja wa wagonjwa hospitalini hapo.
Afisa Utamaduni wa Jiji la Mbeya Nimwindael Mjema akizungumza na wauguzi wa Hospitali ya Wazazi Meta sambamba na wasanii baada ya kutoa msaada.
Waandishi wa habari wakisakata kabumbu na Wasanii wa jiji la mbeya katika sherehe za uzinduzi wa Chama chao
Wasanii wakitoa burudani mbali mbali wakati wa sherehe za uzinduzi wa Chama hichoWASANII wa maigizo na ngoma za asili wametakiwa kuacha tabia ya kuiga tamaduni za nchi za nje na kuzifanyia kazi badala ya kuenzi utamaduni wa Nchi yao kupitia sanaa wanazizifanya.
Mwito huo ulitolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Norman Sigalla ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, wakati wa uzinduzi wa Chama cha Sanaa Jiji la Mbeya(CHASAMBE) uliofanyika katika Viwanja vya chuo cha Uhasibu (TIA) Jijini hapa.
Sigalla alisema sanaa ni kitu pekee kinachoweza kuchangia kudumisha utamaduni wa nchi yoyote kupitia michezo ya kuigiza, kucheza ngoma, uchoraji, ufumaji, uhunzi na ufinyanzi kwa Msanii kuiga vitu vilivyofanyika zamani kwa manufaa ya viziza vijavyo.
Alisema sanaa husaidia kujenga misingi ya watu kufuata misingi na weledi wa utii wa sheria kutokana na wengi wao kuwa katika vikundi mbali mbali hali inayosaidia kuhamasishana kwa manufaa ya taifa jambo ambalo litachangia kuinua dira ya Mtanzania.
Aliongeza kuwa kitendo cha baadhi ya wasanii kuiga utamaduni wa wazungu ni kupoteza maana ya sanaa na kuharibu kabisa utamaduni wa Mtanzania kutokana na watu wanavyotazama kazi za wasanii kwa wingi.
Sigalla alisema kupitia sanaa wananchi wengi hupata ajira kutokana na kazi ya sanaa kutojali umri ambapo Watoto, Vijana na Wazee hujumuika kwa pamoja hivyo husaidia hata kuondoa dhana ya kuwa sanaa ni uhuni.
Kwa upande wake Mlezi wa Chama hicho Jiji la Mbeya, Edna Mwaigomole alisema kazi ya malezi kwa vijana inapaswa kufanywa ni kila mzazi bila kujali nafasi anayokuwa nayo kutokana na umuhimu wa vijana kwa maendeleo ya Taifa.
Naye Mwenyekiti wa Chama hicho, Samweli Mwamboma alisema madhumuni ya kuanzisha chama na kukizindua rasmi ni kutetea maslahi ya wasanii wa sanaa zote.
Aliongeza kuwa madhumuni mengine ni kuhamasisha unndwaji wa vikundi vingi vya sanaa ndani ya jiji la Mbeya, kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa wasanii na kuhamasisha wasanii sanaa kama kazi ya kuwaingizia kipato. kuipenda
Mwenyekiti huyo alisema changamoto kubwa inayowakabili wasanii wa Jiji la Mbeya ni kukosa motisha kutoka kwa baadhi ya wadau ikiwa ni pamoja na serikali kushindwa kuwajengea uwezo kutokana na kuwaita katika shughuli za Kiserikali na kutoa fedha  kidogo isiyoweza kukidhi haja.
Alisema mara nyingi Serikali haiangalii kikundi kinawatu wangapi ambapo baada ya kufanya kazi ya kutoa burudani katika sherehe huambulia malipo ya kati ya Shilingi 30,000 hadi 50,000 wakati kikundi kinakuwa na watu kati ya 15 hadi 40.
Hata hivyo Katibu wa CHASAMBE, Bahati Shulula alisema kutokana na changamoto zinazowakabili wasanii wa Mkoa wa Mbeya kunaongeza kasi ya wasanii wengi kukimbilia Jijini Dar Es Salaam kwa kuamini kuwa fursa nyingi zinapatikana huko.
Alisema Vijana wanafikiri fursa zinazopatikana Dar haziwezi kufika mikoani kama makongamano ya Vijana kutoandaliwa mikoani, kitendo cha Raisi Kikwete kuongea na Wasanii walioko Dar bila kupata wawakilishi kutoka miko yote kinahamasisha kukimbilia huko.

Na Mbeya yetu
Post a Comment