Tuesday, January 14, 2014

HALMASHAURI YA BUSOKELO WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA YAPITISHA MAKISIO KWENYE KIKAO CHA DCC, BAJETI TSH 25,310,697,944.00. BAJETI AMBAYO NI ONGEZEKO LA 59% TOFAUTI NA BAJETI YA MWAKA 2012/2014 AMBAYO BAJETI ILIKUWA TSH 15,892,024,953.00

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIONGOZA KIKAO CHA USHAURI YA HALMASHAURI YA BUSOKELO, MEELA AMEWATAKA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO KUWA MAKINI HASA KUSIMAMINA SUALA LA ELIMU KWANI NDIO MSINGI WA MAENDELEO YA WANNCHI KWANI  MATOKEO YA SASA YA DARASA LA NNE NA DARASA LA SABA NI AIBU KWA BUSOKELO KUFERI KWA KIWANGO CHA AIBU HADI HALMASHAURI YA BUSOKELO KUSHIKA NAMBA YA SITA KWA MKOA WA MBEYA. HIVYO AMEWATAKA WATENDAJI HASA MKURUGENZI NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI KUANGALIA MAPUNGUFU GANI YALIYOSABABISHA KUFERI KWA WATOTO KIWANGO HIKI CHA AIBU SANA "HAIWEZEKANI BUSOKELO WATOTO WAFERI KWA KIASI HIKI KWA KUWA KILA KITU KIPO UKILINGANISHA NA MAENEO MENGINE"

WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA RUNGWE WAKIWASILI KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO WAKIONGOZWA NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MHE, MECKSON MWAKIPUNGA KULIA NA KATIKATI NI MKUU WA WILAYA YA RUNGWE    CHRISPIN MEELA


WAJUMBE WA KIKAO CHA DCC WAKIWA MAKINI KUSOMA KABRASHA ZAO ZA MIPANGO NA BAJETI YA MWAKA 2014/2015

KULIA MRS MWAMTEGELE NA MR MWAKILASA WAKIWA MAKINI KUANDIKA MICHANGO YA WAJUMBE WA KIKAO CHA USHAURI DCC HALMASHAURI YA BUSOKELO


MWENYE TAI NYEKUNDU MR PANJA NA WAJUMBE WA KIKAO WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA USHAURI WA WAJUMBE WA KIKAO CHA DCC HALMASHAURI YA BUSOKELO

BAADHI YA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MWENYE KOTI JEUSI NI KAIMU DT HALMASHAURI YA BUSOKELO MR AIDAN

ALINANUSWE MWAMBUNGU KATIBU WA UDP WILAYA YA RUNGWE AKICHANGIA SUALA LA ELIMU KATIKA HALMASHAURI YA BUSOKELO ILI KUONGEZA UFAURU

WALIO SIMAMA NI MAAFISA WATENDAJI WA KATA ZA HALMASHAURI YA BUSOKELO WALITAKIWA KUSIMAMA NA KILA MTU KUJIELEZA KWANINI HAJAWASILISHA MUHUTASARI YA MIKUTANO MIKUU YA VIJIJI VYAO ILI WAPEWE PESA ZA MIRADI MINGINE. HALMASHAURI YA BUSOKELO IMEWEKA UTARATIBU WA KUTOPELEKA PESA ZA MIRADI KATIKA AKAUTI ZA VIJIJI KABLA YA MREJESHO WA MUHUTASARI UNAOONYESHA MAPATO NA MATUMIZI YA VIJIJI. HIVYO KIKAO KIKAWAPA SIKU KUMI NA NNE KUTEKELEZA MAAGIZO YA KUFANYA KIKAO ILI WANANCHI WAPATIWE PESA ZA MIRADI

MWENYEKITI WA NCCR WILAYA YA RUNGWE MHE, MWASAKILALI AKICHANGIA SEHEMU YA UBORESHAJI WA UKUSANYAJI WA MAPATO HASA KUDHIBITI UTOROSHAJI WA MAZAO KABLA HAYAJALIPIWA USHURU HIVYO HALMASHAURI KUONGEZA UDHIBITI ILI KUONGEZA MAPATO NA WANAOKAMATWA WAKITOROSHA MAZAO KABLA YA KULIPIA WAWAJIBISHWE KISHERIA

MZEE MWAIHOJO AMBAYE NI MWENYEKITI WA TLP WILAYA YA RUNGWE AKIWA MAKINI KUFUATILIA MICHANGO YA WAJUMBE WA KAMATI YA KUSHAURI HALMASHAURI YA BUSOKELO JINSI YA KUTEKELEZA MIPANGO MBALIMBALI YA WANANCHI

MWAKILISHI WA OCD WILAYA YA RUNGWE KAMANDA BULABWA AMEWATAKA WAJUMBE WA KAMATI YA USHAURI YA HALMASHAURI YA BUSOKELO KUENDELEA KUTOA ELIMU YA ULINZI SHIRIKISHI ILI JAMII IISHI KWA AMANI MAANA AMANI HULETA MAENDELEO KATIKA JAMII

AKIZUNGUMZIA MIRADI INAYOTEKELEZWA KATIKA JAMII MHE, MEKSON MWAKIPUNGA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO AMESEMA KUWA IMEFIKA WAKATI SASA WANANCHI WA BUSOKELO KUJIKITA KATIKA UZALISHAJI WA ASALI KWAKUWA BUSOKELO INA KILA SABABU YA KUJIKITA KATIKA KUZALISHA ASALI KWA WINGI ILI KUINUA KIPATO CHA WANANCHI WA BUSOKELO  KWA KUANZIA AMESEMA KUWA HALMASHAURI IMEWEKA MIPANGO YA ELIMU ILIYOANZA KUTEKELEZWA KWA KUWALETA WAKUFUNZI TOKA DODOMA ILI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI HIVYO KWAKUANZIA HALMASHAURI IMEANZAKUTENGENEZA MIZINGA YA NYUKI, MHE,  MWAKIPUNGA  AMEWATAKA WANANCHI MOJAMOJA KUANZA KUWEKEZA KATIKA UFUNGAJI WA NYUKI NA VIJIJI KUWA NA MPANGO HUO ILI KUONGEZA MAPATO YA KIJIJI.

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIHAIRISHA KIKAO CHA DCC HALMASHAURI YA BUSOKELO KWA KUWATAKA WATENDAJI KUJIPANGA KUFANYA KAZI ZA WANANCHI NA KUONGEZA UKUSANYAJI WA MAPATO YA HALMASHAURI YA BUSOKELO ILI KUWA MFANO WA KUIGWA NA WENGI

JENGO LINALOTUMIWA KWA MUDA NA HALMASHAURI YA BUSOKELO AMBALO AWALI LILIKUWA NDIO OFISI YA MBUNGE WA RUNGWE MASHARIKI
HALMASHAURI YA BUSOKELO INAKABILIANA NA CHANGAMOTO LUKUKI KWA KUWA BAJETI IPITISHWAYO SASA NI YA KWANZA TANGU IMEANZISHWA MIEZI MICHACHE ILIYOPITA  HIVYO KWA MUDA MFUPI HADI SASA HALMASHAURI IMESHAMALIZA KUANDAA UPIMAJI WA RAMANI YA ENEO HUSIKA LA BUSOKELO NA KULIPANGIA MATUMIZI HIVYO WADAU NA WAZAWA WANATAKIWA KUCHANGAMKIA FULSA ZA UWEKEZAJI  ZIPATIKANAZO BUSOKELO

SUALA LA AJIRA HALMASHAURI INA WATUMISHI 1O13 HIVYO HALMASHAURI INATARAJIA KUAJIRI WATUMISHI 809 ILI KUONGEZA UFANISI WA KAZI ZA KUWATUMIKIA WANANCHI WA BUSOKELONA WATANZANIA

UTEKELEZAJI WA BEJETI UNATEGEMEANA SANA NA WATENDAJI WA HALMASHAURI KUSIMAMIA PESA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI KUU PAMOJA NA KUKUSANYA MAPATO KWA UADIRIFU PIA SERIKALI KUU KULETA PESA KWA WAKATI NA WANANCHI KUCHANGIA KWA WAKATI PESA ZA MIRADI HUSIKA INAYOTEKELEZWA KATIKA MAENEO YAO

KINGOTANZANIA
Post a Comment