Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya,SACP Ahmed Msangi akizungumza na waandishi wa
habari wa Mkoa wa Mbeya (hawapo pichani) alipowaita kwa kuijitambulisha
kwao na kutoa taarifa ya matukio mbali mbali yaliyotokea kwa kipindi cha
Mwaka 2013.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,SACP Ahmed Msangi
Baadhi ya waandishi wa habari wakiendelea kufuatilia mkutano na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ahmed Msangi
Waandishi
wa habari kutoka vyombo mbali mbali jijini Mbeya wakimsikiliza kwa
makini Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,SACP Ahmed Msangi (hayupo
pichani).
WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
[ASKARI] NA KUSABABISHA KIFO.
MAREHEMU SSGT BENADETHA BONIFASI OLOMI ENZI ZA UHAI WAKE
MNAMO
TAREHE 05.01.2014 MAJIRA YA SAA 12:50HRS HUKO ENEO LA MBEYA ONE, KATA
YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE, BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA. ASKARI EX WP 1601 S/SGT BENADETHA, MIAKA 52,
MCHAGA, ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI TUKUYU WILAYA YA
RUNGWE, AKIWA KAZINI ENEO HILO ALIGONGWA NA GARI T.613 BUM AINA YA
TOYOTA CARINA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ERNEST S/O MATHAYO NDOA,
MMAKUA, MIAKA 35, MKAZI WA KYELA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO
CHA POLISI TUKUYU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUEPUKA MWENDO KASI KWANI NI HATARI NA UNAUA.
Signed by:
[AHMED. Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment