Saturday, January 11, 2014

KKKT DAYOSISI YA ZIWA RUKWA YAPATA ASKOFU WA KWANZA MCH AMBELE MWAIPOPO

ASKOFU MTEULE MCH AMBELE MWAIPOPO AMECHAGULIWA KUWA ASKOFU WA KWANZA WA KKKT DAYOSISI YA ZIWA RUKWA KWA KULA 82 KATI YA WAPIGA KULA 83 WALIO SHIRIKI UCHAGUZI MKUU


ENEO LA MOSSION RUKWA LILIKUWA LINASIMAMIWA NA DAYOSISI TATU ZA KKKT AMBAZO NI DAYOSISI YA KONDE, DAYOSISI YA MAKETE NA DAYOSISI YA MOSHI 

BAADA YA ENEO KUKUA KIHUDUMA YA INJIL,  KKKT IKAPENDEKEA JIMBO LA RUKWA KUWA DAYOSISI MPYA YA ZIWA RUKWA ITAKAYOKUWA NA MAJIMBO MAWILI KWA SASA. HIVYO MKUTANO MKUU UNAOENDELEA CHINI YA MWENYEKITI WA UCHAGUZI, MKUU WA KANISA LA KKKT ALEX MALASUSA HIVYO  MCH AMBELE MWAIPOPO AMECHAGULIWA KUWA ASKOFU WA KWANZA WA DAYOSISI MPYA YA ZIWA RUKWA

KATIKA UCHAGUZI HUO MCH DAVID MASAWE AMECHAGULIWA KUWA MSAIDIZI WA ASKOFU NA KWA UPANDE WA WAKUU WA MAJIMBO, MCH DAVID MOSHI AMECHAGULIWA KUWA MKUU WA JIMBO LA MPANDA NA JIMBO LA SUMBAWANGA LITAONGOZWA NA MCH WILBROD MAGWAYA.

MKUTANO MKUU WA KANISA LA KKT DAYOSISI YA ZIWA RUKWA ULISIMAMIWA NA MKUU WA KANISA ALEX MALASUSA UKIHUDHULIWA NA WAJUMBE WA MKUTANO 83 AMBAO NDIO WAPIGA KULA PIA MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG, STELLA MANYANYA NA MAASKOFU , WACHUNGAJI NA WAGENI MBALIMBALI  WALIOARIKWA KATIKA MKUTANO HUO . MKUTANO UTAHAIRISHWA SIKU YA JUMAPILI BAADA YA IBADA YA KUWEKA WAKFU JIWE LA MSINGI LA KANISA KUU LA KKKT DAYOSISI YA ZIWA RUKWA NA ASKOFU MKUU WA KKKT ALEX MALASUSA

MKUTANO MKUU UNAFANYIKA KWA SIKU NNE KATIKA USHARIKA WA SUMBAWANGA MJINI NA NDIPO MAKAO MAKUU YA DAYOSISI YA SUMBAWANGA YATAKUWA

KINGOTANZANIA
Post a Comment