Ulinzi ukiimarishwa Baada ya watuhumiwa wa ujambazi kufikishwa mahakamani
Mbele ni mshitakiwa wa nne Mbaruku Hamis akiingia mahakamani
Kutoka kushoto ni mshitakiwa wa pili Elinanzi Eliabu Mshana, Mshtakiwa wa nne Mbaruku Hamis, Mshita
mshitakiwa
wa tatu Juma Mussa ambaye aliyekuwa Askari Magereza kwa Cheo cha Sajini
, Anaefuatia ni Mshtakiwa wa kwanza PC James aliyekuwa Askari Polisi
Wilaya ya Mbeya, na wa mwisho ni Mshitakiwa wa Tano Amri Kihenya .
Wa kwanza kushoto aliye vaa shati la Draft ni Dereva Ezekia Matatila (34) pamoja na wasikilizaji
Moja ya Gari lililotumika kufanya uharifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha
Washitakiwa wanne kati ya watano kutoka kushoto juu hadi wa nne wakiwa wanatoka mahakamani chini ya ulinzi mkali.
Mwenye Jaketi la Njano ndiye Mshitakiwa namba moja PC James
Katikati
ni Mke wa mshitakiwa wa tatu ambaye ni Askari Magereza Sajini Juma
Mussa, Hata hivyo mwanamke huyo alizirai mahakamani wakati mumewe akiwa
kizimbani.
**********************************
ASKARI
wawili wa jeshi la Polisi na Magereza pamoja na watu watatu ambao ni
raia wa kawaida wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya
wakituhumiwa kwa ujambazi wa kutumia silaha.
Watuhumiwa
hao watano kwa pamoja walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa
Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Michael Mteite wakituhumiwa kwa kosa moja
la unyang’anyi wa kutumia Silaha kinyume cha Sheria kifungu cha 287 sura
ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni
Mshitakiwa namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye namba
F8302 wa Wilaya ya Mbeya ambaye kabla ya kufikishwa mahakamani alivuliwa
Uaskari baada ya kuhukumiwa kijeshi.
Aliwataja
wengine kuwa ni mshtakiwa namba mbili kuwa ni Elinanzi Mshana(22)Mkazi
wa Iyela Jijini Mbeya, Askari Magereza mwenye namba B 500 Sajenti Juma
Mussa(37) wa Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29) Mkazi wa Iyela na
Amri Kihenya(38) Mkazi wa Iyela.
Akisoma
mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite,
Mulisa alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 3, Mwaka huu
majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya Mbeya
Chunya.
Alisema
watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kulizuia gari aina ya
Pick Up lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34) Mkazi wa Iyunga
Jijini Mbeya ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa jina la
Sreedhar Pasupelet(38) mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo
mawili ambayo ni GX 100 Toyota Cresta T 782 BEU na Gari linguine ambalo
lilikuwa na namba za Chesesi GX 6011832 AINA YA Grand Mark II.
Aliongeza
kuwa mbinu iliyotumika ni watuhumiwa ni watuhumiwa hao kutega magogo
barabarani huku wakiomba msaada kwa madai kuwa magari yao yameharibika
na ndipo baada ya wahanga kusimama waliwapora vitu vyao wakiwa na
mapanga ambavyo ni pesa shilingi Milioni 3.5, Mabegi matatu yenye nguo
mbali mbali yenye nguo, Kompyuta mpakato, simu aina ya Sumsung yenye
thamani ya Shilingi Laki mbili pamoja na simu ya Dereva aina ya Tekno
ambayo aliitambua Mahakani na kutumika kama kielelezo.
Hata
hivyo watuhumiwa wote kwa pamoja walikana kuhusika na matukio hayo
ambapo upande wa Mashtaka ulileta Shahidi mmoja ambaye ni Dereva wa Pick
up Ezekia Matatira ambaye aliwatambua washtakiwa wote watano na
kuiambia mahakama kuwa siku hiyo ya Tukio aliagizwa na Bosi wake kwamba
awapeleke wageni Chunya na ndipo alipotekwa katika eneo hilo huku
watekaji wakiagizwa na Maaskari na yeye kufungwa pingu na kutishiwa na
panga.
Aidha
kutokana na kesi hiyo Hakimu Mteite aliahirisha kesi hiyo hadi Januari
15, mwaka huu ambapo upande wa Mashtaka utaleta mashahidi wengine huku
watuhumiwa wakirudishwa Rumande baada ya dhamana yao kufungwa.
Ezekiel Kamanga
No comments:
Post a Comment