CHAMA cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya
Mbarali Mkoani Mbeya kimemwagia sifa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi
Profesa Annah Tibaijuka kwa uamuzi wake wa kumshinikiza Mwekezaji kampuni
ya Kapunga Rice Project kurejesha shamba lenye ukubwa wa Hekta 1870 kwa
Wananchi.
Pongezi hizo zilitolewa leo na
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Matayo Mwangomo wakati akizungumza na
waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Klabu
ya Waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya(Mbeya press club) zilizopo Soweto Jijini
Mbeya.
Mwangomo amesema kitendo kilichofanywa
na Serikali kupitia kwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka, cha kumtaka Mwekezaji huyo kurudisha sehemu ya ardhi ya wananchi
aliyoichukua kimakosa kitasaidia kumaliza mgogoro uliodumu kati ya Mwekezaji na
wananchi wa kijiji cha Kapunga kwa muda mrefu.
Amesema kutokana na kauli ya hiyo ya
Waziri Tibaijuka imetoa faraja kubwa kwa wakazi wa kata ya Itamboleo kijiji cha
Kapunga ambao walikuwa na mgogoro na mwekezaji huyo tangu mwaka 2006 hivyo
kusababisha wananchi kuishi maisha ya wasiwasi wakihofia kupata madhara kutoka
kwa Makaburu hao ambao ni raia ya Nchini Afrika kusini.
Mwenyekiti huyo ambaye aliongozana na
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (MNEC) kutoka Wilaya ya Mbarali, Geophrey
Mwangurumbi, amesema Mgogoro huo ulianza baada ya Mwekezaji kupewa hati ambayo
ilikuwa na kijiji cha Kapunga ndani yake kimakosa hivyo mgogoro huo unaweza
kuisha kutokana na kauli ya Serikali.
|
No comments:
Post a Comment