Wednesday, January 29, 2014

MKUNGA WA JADI ALIYEFANIKIWA KUMZALISHA MWANAMKE WATOTO WATATU AOMBA MSAADA WA VIFAA VYA KUZALISHIA

Mkunga wa jadi Bi Dotea Mwanakulya 60 wa kijiji cha magamba Chunya akimpokea mgonjwa aliyekuja kujifungua aitwae Kundu Luhende 20 

Mkunga huyo wa alisema anakabiliwa na changamoto za ukosefu wa vifaa vya kujifungulia kama kitanda,godoro,mipira ya kuvaa mikononi ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa ambapo wagonjwa wengine hufika hapo wakiwa hawana vifaa  hivyo.

Mkunga wa jadi Bi Dotea Mwanakulya 60 wa kijiji cha magamba Chunya akiandaa mazingira ya kujifungulia mjamzito

Mkunga wa jadi Bi Dotea Mwanakulya 60 wa kijiji cha magamba Chunya akiwa na msaidizi wakeBi Flora Steven

Hii ndiyo nyumba ya kujifungulia wajawazito kijijini hapo

Mkunga wa jadi Bi Dotea Mwanakulya 60 wa kijiji cha magamba Chunya akiwa na mumewe kulia Emili Sele 77 na mjukuu wake kushoto

Hii ni nyumba ya mama mkunga  ndimo anamoishi

Paskalia Adorf akiwa na watoto watatu aliojifungua kwa wakati mmoja na wanawe wengine na mmoja hayupo pichani 

Paskalia amejifungua watoto wawili jinsi ya kiume na mmoja wa kike ambapo amesaidiwa  na mkunga wa jadi  Dotea Mwanakulya (60)anayeishi kijiji cha Magamba



WADAU wa sekta ya Afya nchini wametakiwa kuwajali na kuwathamini wakunga wa Jadi kwa kuwa wamekuwa wakombozi kwa wazazi waishio mbali na vituo vya afya pindi wanapohitaji huduma ya kujifungua.
Mwito huo ulitolewa na Mkunga wa Jadi, Dotea Mwanakulya (60) Mkazi wa kijiji cha Magamba Wilayani Chunya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea nyumbani kwake kujua changamoto anazokabiliana nazo.
Mkunga huyo wa alisema anakabiliwa na changamoto za ukosefu wa vifaa vya kujifungulia kama kitanda,godoro,mipira ya kuvaa mikononi ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa ambapo wagonjwa wengine hufika hapo wakiwa hawana vifaa  hivyo.
Hata hivyo mkunga huyo amewaomba wadau mbali mbali kumsaidia kupata daftari ya kutunza kumbukumbu za watoto wanaozaliwa nyumbani kwake kwa kile alichodai kuwa hana kumbukumbu sahihi za idadi hali ya watoto waliozaliwa kwake.
Mkunga huyo alilazimika kutoa kauli hizo kufuatia kuwepo kwa Mwanamke mmoja kujifunga watoto mapacha mfululizo kwa Mkunga huyo na watoto wake wakiendelea kukua vizuri.
Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Paskalia Adrofu (37)mkazi wa kijiji cha Magamba kata ya Magamba wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya,alijifungua salama watoto watatu hivi karibuni kwa mkunga wa Jadi huyo.
Paskalia amejifungua watoto wawili jinsi ya kiume na mmoja wa kike ambapo amesaidiwa  na mkunga wa jadi  Dotea Mwanakulya (60)anayeishi kijiji cha Magamba.
Paskalia alisema kwamba mume wake aitwaye Richard Saba (55) ni mkulima hivyo imekuwa vigumu kwake kumudu gharama za matunzo kwa watoto hao ambapo ana jumla ya watoto wanane,wakiwemo mapacha ambao wamemaliza shule ya msingi na hawajachaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari.
Mama huyo alianza kujifungua mtoto wa kwanza mwaka 1995,wa pili ambao ni mapacha mwaka 1998 wa tatu mwaka 2006,wa nne mwaka 2009 na wa tano ambao wamezaliwa watatu amejifungua mwanzoni mwa mwaka huu ambao wana afya njema.
Hata hivyo Paskalia alisema uongozi wa kata akiwemo Diwani wa kata ya Magamba  Chakupewa Kapalala wamefika kumtembelea na kumjulia hali yake na kumhimiza kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili kufuatilia afya za watoto.
Aidha mkazi mmoja wa kijiji hicho aitwaye Luhende Luhaga ametoa ng’ombe wawili wa maziwa ili mama huyo amudu kuwanyonyesha watoto hao bila shida kutokana na kulemewa na watoto hao.
Watoto wawili wa mwanzo wamezaliwa na uzito wa kilo 2.8 na wa tatu amezaliwa na uzito wa kilo 2.0 ambapo Paskalia alisema kuwa watapofikia uzito wa kilo 3 ndipo watapatiwa chanjo katika zahanati ya Magamba.
Baadhi ya changamoto anazokabiliwa nazo ni pamoja na nguo za watoto,chupa za kunyonyeshea,sabuni,mafuta na chupa za chai kwa ajili ya kuhifadhia maziwa ya watoto.
Na Ezekiel Kamanga

No comments: