Thursday, January 30, 2014

BUSOKELO WAJIPANGA NA MKAKATI WA KUBORESHA ELIMU ILI KUONGEZA UFAURU WA WANAFUNZI PIA UKUSANYAJI WA KODI ILI KUONGEZA MAPATO YA HALMASHAURI NA KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI YA WANANCHI WA BUSOKELO WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA

KATIKATI MHE, MECKSON MWAKIPUNGWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA RUNGWE AKIWA NA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA NA KAIMU MKURUGENZI WA WILAYA YA RUNGWE FOLKWARD MCHAMI WAKIINGIA KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI TAYARI KWA KUANZA KIKAO CHA KAZI CHA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA BUSOKELO
MHE, MECKSON MWAKIPUNGA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO AKIFUNUA KIKAO NA KURUHUSU AJENDA ZIPATAZO KUMI KUJADILIWA KWA MAKINI KATIKA KIKAO HIKI CHA KAWAIDA CHA KAZI AMBAPO CHANGAMOTO KUBWA KATIKA KIKAO HIKI NI KUPOROMOKA KWA ELIMU NA MATOKEO MABAYA YA DARASA LA SABA KUSHIKA NAMBA SITA TOFAUTI NA RUNGWE AMBAYO NI YA PILI KIMKOA  NA DARASA LA NNE BUSOKELO KUSHIKA NAMBA NNE TOFAUTI NA RUNGWE ILIYOSHOKA NAMBA MOJA KIMKOA
AJENDA ZIKAAZA KUPITIWA MOJA BAADA YA NYINGINE
WAHESHIMIWA MADIWANI WAKIWA MAKINI KUSOMA HATUA KWA HATUA NA KUJADIRI MASUALA MUHIMU YA KUJENGA HALMASHAURI YA BUSOKELO



WATENDAJI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO WAKIWA MAKINI KUFUATILIA MAJADARA NA MAWAZO YA WAJUMBE KATIKA KIKAO HIKI CHA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA BUSOKELOAMBAPO WAKUU WA IDARA WAMETAKIWA KUSIMAMIA IDARA ZAO KWA KUWA WAZALENDO WA MAENDELEO YA WANANCHI WA BUSOKELO NA KWA WATANZANIA

KUSHOTO MR MALCK PANJA AFISA UGAVI BUSOKELO  NA MR

CHANGAMOTO KUU YA KUPOROMOKA KWA ELIMU MHE, KOMBOTEKA AKASEMA KWA KUWA KUNA UKOSEFU WA WALIMU NA VITENDEA KAZI LAKINI TATIZO KUBWA LINALO IKABIRI HALMASHAURI YA BUSOKELO NI MTENDAJI MKUU WA IDARA YA ELIMU MSINGI IRENE  MAKUNGU, KUTOSIMAMIA IDARA YAKE AMBAPO AMEKUWA NI MTU WA KUKWEPA VIKAO VYA MSINGI KAMA BARAZA LA MADIWANI SASA YAPATA KIKAO CHA NNE NA HATA KIKAO CHA BAJETI HAJASHIRIKI HUKU HATA SIKU ZA KAZI NI SHIDA KUMKUTA OFISIN HIVYO MTUMISHI HUYU ATAONGOZAJE IDARA NA IKAWA NA MATUNDA MAZURI YA KUFAURU WATOTO WETU?

MHE, MWASOMOLA AMESEMA KUWA MKUU WA IDARA YA ELIMU MSINGI IRENE MAKUNGU HAFAI KUWA MTUMISHI WA BUSOKELO KWA KUWA YEYE KILA SIKU NI SAFARI NA KUTOKUWEPO KAZINI ZAIDI NI SHIDA YA KUTOHUDHULIA VIKAO VYA MUHIMU


ANNA MWAMTEGELE AMBAYE NI MWANDISHI WA VIKAO VYA HALMASHAURI YA BUSOKELO AKIWA MAKINI KUANDIKA YALE YOTE YANAYOZUNGUMZWA NA WAJUMBE WA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI

MADIWANI WA BUSOKELO WAKIWA MAKINI KATIKA KUJADILI MAMBO MUHIMU YA WANANCHI AMBAPO WATENDAJI WAMEKEMEWA KUWA WAADILIFU KATIKA KUSIMAMIA MIRADI MBALIMBALI INAYOTEKELEZWA NA KATIKA JAMII

MHE, TWISILE MWALUGAJA PIA AMEKEMEA TABIA YA MKUU WA IDARA AMBAYE NI MWANAMKE IRENE MAKUNGU AMBAPO AMESEMA KUWA IRENE KAMA MTUMISHI WA IDARA TENA MWANAMKE AMEIANGUSHA HALMASHAURI YA BUSOKELO KWA KUWA ILIMWAMINI KAMA ATASIMAMIA IDARA VYEMA SASA NI KINYUME NA MADARAJIO HALMASHAURI KUTAALUMA IMEPOROMOKA HIVYO PAMOJA NA MAONYO MENGI KWA MTUMISHI HUYO NA WENGINE WENYE TABIA KAMA ZAKE, SASA IMEFIKIA HATUA YA MWISHO YA KUCHUKUA HATUA NYINGINE

MHE, SALOME MAKAMU MWENYEKITI WA BUSOKELO AKIONGEA KATIKA KIAO
AKITOA TAARIFA YA SERIKALI HUKU AKIGUSIA  MAMBO MENGI YA ETEKELEZAJI  WA MIRADI NA UKAGUZI WAKE, MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AMEKEMEA SANA TABIA YA BARAZA LA MADIWANI KUWA BARAZA LA KULALAMIKA NA KUWALALAMIKIA WATUMISHI WAO KUWA HAWAFANYI KAZI WAKATI WAO NDIO WAAJIRI WA WATUMISHI WAO WOTE. HIVYO AMEWATAKA MADIWANI WA BUSOKELO KUCHUKUA HATUA KWA WATENDAJI WOTE WASIO WAADIRIFU KATIKA KUTENDA MAJUKUMU YAO YA KAZI, PIA AMEWATAKA MADIWANI KUPITIA MKURUGENZI WA BUSOKELO KUTAKA IFIKAPO JUMATATU ANATAKA RIPOTI YA HATUA MADHUBUTI ZILIZOCHUKULIWA KWA WATUMISHI WASIO WAADILIFU KWA KUANZIA MKUU WA IDARA YA ELIMU AMBAYE AMELALA MIKIWA KUWA NI MTU ASIYEHUDHULIA VIKAO NA KUSAFIRI BILA YA KUPEWA RUHUSA PIA KUSABABISHA IDARA YAKE KUTOFANYA VIZURI

AKIFUNGA KIKAO MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO AMEWATAKA WATENDAJI KUFANYA KAZI ZA WANANCHI AMBAZO WANATAKIWA KUWAJIBIKA KUZIFANYA ILI WANANCHI KUWA NA MAISHA BORA PIA AMEWATAKA MADIWANI KUWA CHACHU YA KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA MAPATO KATIKA KATA ZAO ILI KUONGEZA TIJA YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA BUSOKELO AMBAYO HADI SASA MAFANIKIO YAMEANZA KUONEKANA JAPO NI MUDA MFUPI SANA TANGU HALMASHAURI KUANZISHWA OKTOBA MWAKA 2012

KINGOTANZANIA -  0752881456


No comments: