Thursday, January 30, 2014

MAZISHI YA BOAZI MBINILE YAFANYIKA KIJIJINI KWAKE SIMIKE WILAYANI RUNGWE MAZIKO YALIYOONGOZWA NA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA

MSAFARA WA MAZIKO YA BOAZI MBINILE MTUMISHI WA HAZINA WILAYANI RUNGWE ALIYEFARIKI KWA AJLI YA GALI AKITOKEA MBEYA AMBAKO ALIKWENDA KIKAZI KATIKA OFISI ZA CAG AMBAPO ALIPELEKA TAARIFA ZA HESABU ZA HALMASHAURI YA RUNGWE ALIPOKUWA ANARUDI WILAYANI RUNGWE KUFIKA ENEO LA SHULE YA KIPOKE SEKONDALI KIWIRA  DARAJANI KWA MBELE KUNA KONA NDIPO GALI ALILOKUWA ANAENDESHA LILIPATA AJALI NA BOAZI KUKIMBIZWA KATIKA HOSPTALI YA TUKUYU KWA MATIBABU LAKINI BAADA YA MASAA MACHACHE BOAZI MBINILE AKAAGA DUNIA. HIVYO MSAFARA HUU UMETOKA NYUMBANI KWAKE KATUMBA KUELEKEA SEHEMU YA MAZIKO KIJIJI CHA SIMIKE WILAYA YA RUNGWE
PICHA INAYOMUNYESHA BOAZI MBINILE ENZI YA UHAI WAKE

IBADA YA MAZIKO IKIONGOZWA NA KKKT USHARIKA WA KATUMBA

KATIKATI NI MKE WA MAREHEMU BOAZI MBINILE AKIWA MTU WA MAJOZI KATIKA KUSHIRIKI MAZIKO YA MUMEWE ALIYEFARIKI KWA AJALI YA GALI AKIWA SAFARINI TOKA MBEYA AKILEJEA NYUMBANI

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIONGOZANA NA VIONGOZI WENZAKE WA CHAMA NA SERIKALI KATIKA KUWAONGOZA MAMIA YA WANANCHI WA WILAYA YA RUNGWE NA VITONGOJI VYAKE WAKISHIRIKI MAZIKO YA BOAZI MBINILE KIJIJINI KWAO SIMIKE WILAYANI RUNGWE

MCHUNGAJI WA KKKT USHARIKA WA KATUMBA AKIONGOZA IBADA YA MAZIKO YA BOAZI MBINILE AMBAPO MCHUNGAJI AMESEMA KIFO NI NJIA YA KILA MTU KUIPITIA HIVYO SUALA LA MSINGI KUJIANDAA KWA KUTENDA MEMA DUNIANI YEMPENDEZAYO MUNGU KWA KUWA HAKUNA MTU YEYOTE AJUAYE SIKU WALA SAA YA KUFA

MWENYEKITI WA HALAMSHAURI YA RUNGWE AKITOA SALAMA ZA LAMBILAMBI ZA HALMASHAURI YA RUNGWE AMBAPO MHE AMESEMA KUWA HALMASHAURI YA RUNGWE IMEMPOTEZA MTU AMBAYE ALIKUWA NI KIUNGO NA MTENDAJI BORA WA MAJUKUMU ALIYOPANGIWA HASA KATIKA KITENGO CHAKE CHA MAPATO

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AMESEMA KUWA WATUMISHI WALIOWENGI WAKIPATA NAFASI WANAKOSA UADILIFU KATIKA KAZI ZAO LAKIN HAIKUWA HIVYO KWA BOAZI MBINILE AMBAPO BOAZI BILA YA KUUMA MANENO ALIKUWA MTU ALIYEKUWA NI MZALENDO KATIKA KULITUMIKIA TAIFA LAKE NA WILAYA YA RUNGWE KWA KUKUSANYA KODI BILA YA KUOGOPA VITISHO. HIVYO KWA KUTAMBUA MCHANGO WA BOAZI MBINILE SERIKALI IMEAHIDI KUPEFIKISHA MRADI WA UMEME KIJIJINI HAPO IKIWA NI KUUENZI MCHANGO WA MAREHEMU KATIKA UTENDAJI WAKE MZURI WA KAZI

MWAKILISHI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MR AIDAI AMBAYE AWALI ALIKUWA NI MFANYA KAZI WA RUNGWE AKIWASILISHA SALAM ZA LAMBILAMBI KUTOKA HALMASHAURI YA BUSOKELO


ANAYEONGEA NI MUWAKILISHI WA CHUO KIKUU CHA MZUMBE TAWI LA MBEYA AMBAPO MAREHEMU BOAZI MBINILE ALIKUWA NI MWANAFUNZI WA SHAHADA YA PILI YA UZAMILI YA UTAWALA WA BIASHARA AMBAPO ALIKUWA HATUA ZA MWISHO KUMALIZA MASOMO YAKE

MUWAKILISHI WA JESHI LA POLISI WILAYA YA RUNGWE AKITOA SALAM ZA LAMBILAMBI AMBAPO AMEWATAKA HASA VIJANA KUIGA MFANO WA BOAZ MBINILE KUWA MTU ANAYE PENDA AMANI KATIKA KAZI NA JAMII

KATIBU MWENEZI WA CCM WILAYA YA RUNGWE MHE, MAKALA AKITOA SALAM ZA LAMBILAMBI AMBAPO AMESEMA HAKUNA MTU WILAYANI RUNGWE ASIYEJUA MCHANGO WA MBINILE KATIKA KUKUSANYA MAPATO HIVYO CCM WILAYA YA RUNGWE KWA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KATIKA KUTEKELEZA ILANI YA CHAMA BASI CCM ITATOA ADA YA SHULE KWA  MTOTO MMOJA WA MAREHEMU BOAZI

KATI YA WATU WALIOTOA SALAM ALIKUWEPO NA ASKOFU MSAIDIZI MSTAFU WA KKKT AMBAYE ALIWAKILISHA KANISA NA BODI YA SHULE YA SEKONDALI YA LUPOTO  MCH KAPULA AMESEMA BOAZ AMEKUWA MTU WA KUAMINIKA KANISANI KAZINI KWAKE HATA KWENYE JAMII HIVYO TUNATAKIWA KUENZI MCHANGO WAKE KWA KUYAENDELEZA MEMA ALIYOTUACHIA

MR C. NYANYEMBE AMBAYE MWENYEKITI MSTAFU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MBEYA YEYE NI SHEMEJI YAKE NA MAREHEMU

JENEZA LILILOBEBA MWILI WA MAREHEMU BOAZI MBINILE LIKIINGIZWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

WAKATI JENEZA LIKIWEKWA KATIKA NYUMBA YA MILELE NI WAKATI MGUMU SANA KWA MKEWE NA WATOTO PIA NDUGU KUSHUHUDIA HILI


MKWE WA MAREHEMU AKISAIDIWA KUWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA MUMEWE

WATOTO WA MAREHEMU KWA PAMOJA WAKISHIRIKIANA KUWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA BABA YAO

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE AKIWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA BOAZI MBINILE IKIWA NI ISHARA YA UPENDO NA UWAKILISHI WA WANANCHI WOTE WA WILAYA YA RUNGWE

KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA RUNGWE GWABO MWANSASU AKIWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA MTUMISHI WAKE BOAZI MBINILE

WA PILI KULIA NI MR MWANKEJELA AKIWAONGOZA WAFANYA KAZI WENZAKE WA IDARA YA UHASIBU WAKIWEKA MASHADA YA MAUA KATIKA KABURI LA MFANYAKAZI MWENZAO
KATIKATI NDIO BABA WA MAREHEMU BOAZI MBINILE  MZEE MBINILE AKIWA NA MTOTO WA MAREHEMU WAKIWA NA MAJONZI YA KUTOAMINI KINACHOENDELEA

MUWAKILISHI WA FAMILIA YA MZEE MBINILE WA KATUMA AKIONGEA NAKUTOA SHUKRANI ZA PEKEE KWA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI HASA VIONGOZI WA SERIKALI NA HALMASHAURI PAMOJA NA CHAMA ZAIDI VIJANA WA LIOSHIRIKI KUCHIMBA KABURI AMBAMO AMEZIKWA BOAZI MBINILE PIA AMEWASHUKURU KIPEKEE WACHUNGAJI WA KANISA LA KKKT NA KWAYA ZOTE PAMOJA NA WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA MAZIKO YA NDUGU YAO MPENDWA BOAZI ZAIDI AMEOMBA UPENDO ULIOTAWALA KATIKA MAZIKO HAYA NA UENDELEE KATIKA KUMTUNZA MJANE NA WATOTO HASA KUWAENDELEZA KIELIMU

BAADA YA MAZIKO WATU WANASHIRIKI CHAKULA AINA YA KANDE (NGATI NDETA NI NDUNDU)
 MAREHEMU AMEZALIWA TAREHE 11.11.1974 NA ALIAJIRIWA HALMASHAURI YA RUNGWE MWAKA 2003 NA HADI MAUTI INAMKUTA MAREHEMU BOAZI ALIKUWA MTUMISHI WA HALMASHAURI YA RUNGWE KITENGO CHA MAPATO . MAREHEMU BOAZI AMEFARIKI KWA AJALI YA GALI TAREHE 29.01.2014NA KUZIKWA KIJIJINI KWAKE SIMIKE WILAYANI RUNGWE. MAREHEMU BOAZI MBINILE AMEACHA MJANE MMOJA NA WATOTO WATATU.



No comments: