Serikali imetangaza neema kwa vijiji
vinavyopitiwa na bomba la gesi ambavyo vipo mkoani Mtwara na Lindi, sasa
wataunganishiwa kwa Sh27,000.
Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mbele ya Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda kwenye uzinduzi mradi wa umeme wilayani Nanyumbu na
Masasi.
Profesa Muhongo alisema gharama za kuunganisha umeme kwa sasa ni Sh177,000.
Alisema zaidi ya vijiji 50 vimepewa upendeleo huo ili kuwawezesha wananchi kuwa na maisha bora.
Lengo la Serikali ni kufikia asilimia
30 ya wasasatu waliounganishwa na umeme na kwamba, hivi sasa ni asilimia
23 pekee wanaopata umeme nchini wakati Mtwara ni asilimia nne.
Kuhusu umeme wa gesi, Profesa Muhongo
alisema Mtwara wanatarajia kuzalisha megawati 600 ambazo baada ya
matumizi nchini, zitauzwa nchi za Malawi, Zambia na Msumbijj.
Awali, akizungumza na mamia ya wakazi
wa Mangaka waliofika kushuhudia uzinduzi huo, Pinda alisema mradi huo ni
utekelezaji wa azma ya Serikali kuhakikisha kila wilaya inapata umeme.
"Mpango wa kupeleka umeme nchini ni wa
miaka mitatu na katika sekta ya nishati chini ya Mpango wa Matokeo
Makubwa ya Sasa (BRN), tumeazimia kwenda kwa awamu," alisema.
ili tuwafikie wananchi wengi zaidi
kutoka asilimia 24 ya sasa hadi kufikia asilimia 30 ya watumiaji wa
umeme," alisema Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment