Mkurugenzi
wa Takwimu za Uchumi Bw. Morice Oyuke kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(katikati) akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa Pato la
Taifa kwa robo mwaka ya tatu ya mwaka 2013 ambapo katika kipindi cha
Julai – Septemba, 2013 Pato la Taifa kwa bei za soko liliongezeka kwa
kasi ya asilimia 6.5 ikilinganishwa na asilimia 7.2 kwa kipindi kama
hicho mwaka 2012. Kulia kwake ni Bw. Juma Omary, Mchumi Mkuu kutoka
Ofisi ya Rais Tume ya Mipango na kushoto ni Bw. Daniel Masolwa Meneja
Takwimu za Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi
Bw. Morice Oyuke kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) akizungumza
kuhusu ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo mwaka ya tatu ya mwaka 2013
katika ukumbi uliopo Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment