Saturday, January 25, 2014

Waziri Mkuu awaasa wanachi kutunza miundo mbinu ya mradi wa gesi nchini.

1 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na mafundi wanaojenga bomba la mradi wa gasi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua mradi huo.
 2 
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akieleza hatua iliyofikiwa katika ujennzi wa bomba la gasi linalojengwa kutoka Mtwara hadi Dar es salaam kwa Waziri Mkuu na msafara wake. Kushoto ni Balozi wa China nchini, Lu Younqing. 3 
Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akimsikiliza Waziri wa Nishati na Prof. Madini Sospeter Muhongo akizungumzia ujenzi wa bomba la gasi eneo la Bungu mkoa wa Pwani. 4 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na msafara wake wakiangalia eneo utakapochimbwa mtaro wa kupitishia bomba la gesi. 5 
Mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha mabomba kabla ya kuyalaza na kuyafukia chini kwenye mitaro 6 
Mkuu wa mkoa wa Lindi akiwa na Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili mkoani humo na kuendelea na ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi 7Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha MEIS Merea Barabuu akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo eneo la Machole Mkoani Lindi. 8 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi na wafanyakazi wa ujenzi kiwanda cha MEIS faida zitzkazotokana na kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa gasi kijijini hapo kwa njia rahisi baada ya kuunganishwa kutoka bomba kuu la gasi ikiwemo ajira kwa wananchi na upatikanaji wa saruji kwa bei nafuu ili kuboresha makazi yao. 9 
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha MEIS kilichopo eneo la Machole Mkoani Lindi. 10 
Picha ya sura na muonekano wa kiwanda cha MEIS kitakapokamilioka
……………………………………………………………………………………..

SERIKALI imewapa jukumu wananchi wanaoishi maeneo linapopita  bomba la kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam la kulitunza na kulilinda  kwa manufaa yao na taifa zima.
Wito huo ulitolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda  leo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba hilo.
Waziri Mkuu Pinda alisema Serikali inavihakikishia vijiji lilipopita bomba hilo kuwa watapatiwa umeme unaotokana na uzalishaji wa gasi na utakuwa wa gharama nafuu.
Zaidi ya hayo, gasi itatumika kwa matumizi ya nyumbani kwa kuunganishiwa bomba la gasi na ambao hawatafanikiwa watakuwa na fursa ya kupata mitungi ya gesi ambayo itakuwa ya bei nafuu.

Waziri Mkuu ameagiza mashirika ya Shirika la gasi na Petroli Tanzania (TPDC) na Mradi wa Nishati Vijijini (REA) wachukue jukumu la kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo lilipopita bomba hilo katika maeneo ya barabara, shule, kuwapatia maji safi na salama,kuwaboreshea utoaji wa huduma za afya kwa kuboresha zahanati na vituo vya afya kama mchango wao kwa jamii.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alisema kuwa serikali kupitia shirika la TPDC na REA itahakikisha wanachi waishio vjijini wanapata umeme mapema iwezekanavyo.

Kwa kuthibitisha kauli hiyo Prof. Muhongo alisema serikali kupitia TPDC na REA imetenga sh. Bilioni 20 kwa awamu ya kwanza ambayo itasimamiwa na REA wakati awamu ya pili nayo itatumia bilioni 20 iotkaysimamiwa na TPDC.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu aliambatana na mke wake bi Tunu Pinda, Balozi wa China nchini, Lu Younqing, Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, mbunge wa Mchinga Said Matanda na Fatma Mikidadi mbunge wa viti maalum.
Maeneo aliyotembelea Waziri Mkuu ni pamoja na Vikindu, Jopika, Bungu, Ikwiriri, Somanga, Somanga Fungu, Kitomanga na Lindi.

Na Eleuteri Mangi-Maelezo Mtwara


No comments: