Ugunduzi huu umepelekea Wizara ya Nishati na Madini kupokea
wageni wanaowakilisha nchi na watu binafsi wanaofika ili kutafuta fursa za
kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano ya kibiashara baina ya
nchi husika.
Hivi karibuni wizara ya
Nishati na Madini imetembelewa na ujumbe toka Jamuri ya Czech nchi ndogo
miongoni mwa nchi zinazounga umoja wa ulaya waliofika kwa lengo la kutafuta
fursa za kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kudumisha uhusiano baina ya nchi
hizi mbili.
Ujumbe huu uliongonzwa na Bw. Tomas Dub Naibu Waziri wa mambo ya Nje ya
Nchi ya Czech aliyeelezea uwezo wa nchi yake katika masuala ya nishati na
madini na kusema kwamba awali nchi yao ilijikita katika umeme uliozalishwa kwa
maji, gesi pamoja na nishati jadidifu,
na kusema kwamba wana wataalamu wa kutosha katika sekta ya nishati.
Dub alieleza kuwa maendeleo si tu kutegemea utafutaji na
uzalishaji wa gesi asilia bali inatakiwa nchi ifanye nguvu ya ziada katika
kuongeza thamani ya bidhaa hiyo na hilo litawezekana tu kwa kujenga viwanda
jambo lililowavuta ili kuja kutafuta fursa hiyo nchini.
Dub alikamilisha mahojiano hayo kwa kuitaka Wizara kuelimisha watanzania katika chuo cha madini
katika nchi hiyo na kwamba mawasiliano yataendelea kufanyika ili kufikia
malengo ya uhusiano huo.
Kwa upande wake Masele amesema kwamba zipo fursa nyingi za uwekezaji nchini katika sekta ya
madini na zaidi madini ya viwandani
lakini pia sekta ya nishati kwa kufuatia ugunduzi wa gesi na mafuta vitalu
vimetangazwa hivyo ni fursa kwa Czech kuomba vitalu hivyo ili kuweza kushiriki
katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi.
Na Nuru Mwasampeta
No comments:
Post a Comment