Tuesday, January 21, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DV7A3218 
WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 20.01.2014 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA –TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. DAINA D/O KIHABA, MIAKA 80, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA SYUKULA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.  MAREHEMU ALIJERUHIWA KWA KUKATWA PANGA KICHWANI NA MIKONONI TAREHE 19.01.2014 MAJIRA YA SAA 21:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA SYUKULA, KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE NA HOSEA S/O MWAISWELO, MIAKA 20, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA SYUKULA.  CHANZO KINACHUNGUZWA HATA HIVYO UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA MTUHUMIWA ANA MATATIZO YA AKILI. MBINU NI KUMVAMIA MAREHEMU AKIWA NDANI YA  NYUMBA ANAKULA CHAKULA NA MJUKUU WAKE  ESTER D/O KITWIKA, MIAKA 9, KYUSA, MWANAFUNZI S/MSINGI SYUKULA STD IV AMBAYE ALIJERUHIWA NA KUPATIWA MATIBABU KISHA KURUHUSIWA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII PALE WANAPOKUWA NA MGONJWA/WAGONJWA WA AKILI NI VIZURI KUHAKIKISHA ANAPELEKWA HOSPITALI KUPATIWA TIBA ILI KUEPUSHA MADHARA YA AINA YOYOTE KWAKE NA KWA JAMII NZIMA.

WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA MOTO.
MNAMO TAREHE 21.01.2014 MAJIRA YA SAA 01:00HRS HUKO ENEO LA MWANJELWA, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. MFIKEMO S/O OSIA, MIAKA 50, KYUSA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA BLOCK Q ALIGUNDUA KUUNGUA MOTO KWA VYUMBA VIWILI VYA MADUKA YA  NGUO MALI YA  WAPANGAJI WAKE WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA JINA MOJA MOJA  VICK D/O ? NA MELELE S/O ? NA KUSABABISHA MALI YOTE KUTEKETEA. DUKA HILO LINA JUMLA YA VYUMBA VITANO. CHANZO BADO KUFAHAMIKA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA HAIJAFAHAMIKA. HAKUNA MADHARA YA  KIBINADAMU YALIYOTOKEA. MOTO HUO ULIZIMWA NA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA KUSHIRIKIANA NA POLISI NA WANANCHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI KWA KUCHUKUA TAHADHARI YA MAJANGA YA MOTO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA.

WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA UPEPO.Add caption

MNAMO TAREHE 20.01.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA VITONGOJI VYA MLIMA RELI, CHAPAKAZI NA MTAKUJA VILIVYOPO KATA YA  UTENGULE USONGWE, TARAFA YA  BONDE LA SONGWE,  WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. UPEPO MKALI [KIMBUNGA] ULIOAMBATANA NA MVUA ULISABABISHA ATHARI KUBWA KWA KUEZUA MAPAA YA NYUMBA 15 ZA KUISHI WATU, VIBANDA VYA BIASHARA 18 NA KANISA MOJA EAGT. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYOTOKEA. THAMANI HALISI YA UHARIBIFU BADO KUFAHAMIKA IKIWA NI PAMOJA NA IDADI KAMILI YA FAMILIA ZILIZOATHIRIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment