……………………………………………………………………………………..
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Mheshimiwa Perseko Kone kutokana na vifo vya watu wazima 12 na mtoto
mmoja wa miezi minne vilivyotokea tarehe 20 Januari, 2014 kufuatia
kugongana uso kwa uso kwa gari aina ya Toyota Noah lililokuwa limebeba
abiria likitokea Itogi kwenda Singida na lori katika eneo la Isuna
Mkoani Singida.
“Nimeshtushwa,
nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya watu 13
akiwemo mtoto wa miezi minne waliofariki papo hapo katika eneo la ajali
tarehe 20 Januari, 2014 baada ya gari aina ya Toyota Noah walilokuwa
wakisafiria kutoka Itigi kwenda Singida kugongana uso kwa uso na lori
katika eneo la Isuna”.
Rais Kikwete
amesema inatia simanzi kuona ajali zikiendelea kutokea na kupoteza
maisha ya watu wasio na hatia na hususan mtoto mdogo kama huyu wa miezi
minne, kusababisha ulemavu wa kudumu kwa baadhi ya watu na uharibifu wa
mali kutokana na makosa ya binadamu katika uendeshaji wa vyombo vya
moto.
“Kufuatia
ajali hiyo ya kusikitisha, ninakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Mheshimiwa Perseko Kone salamu zangu za rambirambi kutokana na msiba
huo, na kupitia kwako, naomba unifikishie salamu zangu za rambirambi na
pole nyingi kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao katika ajali
hiyo. Nawaomba wanafamilia wawe na moyo wa uvumilivu, subira na ujasiri
hivi sasa wanapougulia machungu ya kupotelewa na ndugu zao”, amesema Rais Kikwete kwa masikitiko.
Aidha
Rais Kikwete amesema anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema
azipokee na kuzilaza Mahala Pema Peponi Roho za Marehemu wote, na
amewahakikishia wafiwa kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba huu
mkubwa.
Vilevile
amemtakia ahueni kijana mmoja majeruhi wa ajali hiyo na aweze kupona
haraka na kurejea katika hali yake ya kawaida na kuungana tena na ndugu
na jamaa zake.
No comments:
Post a Comment