Fundi mitambo Daniel Mwakamala akiwa kazini na mtambo wa kusindilia uwanja |
Mwendesha mtambo Daniel Mwakamala akisindilia Uwanja wa Sokoine wakati wa ukarabati wa uwanja huo ambao ulifungiwa na TFF kutokana na kutokodhi viwango. |
Hatimaye kilio cha Wapenzi wa Soka mkoani Mbeya na mikoa ya jirani
kinakaribia kumalizika baada ya kuwepo na matumaini ya kukamilika kwa
Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine ambao ni miongoni mwa viwanja vinane
vilivyofungiwa kutochezeshwa mechi za Ligi kuu kutokana na hali ya
uwanja huo kutoridhisha.
Jitihada za serikali ya Mkoa wa Mbeya
na wadau wa soka wakiwemo Chama Cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mbeya MREFA
kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Jeshi la Magereza na
Jeshi la Kujenga Taifa (JWTZ) uwanja huo umekamilika kwa zaidi ya
asilimia 80.
Kwa mujibu wa taarifa za Mwenyekiti
wa Chama Cha Mpira wa miguu mkoa wa Mbeya Elias Mwanjala ukarabati wa
uwanja huo umefikia zaidi ya sh. milioni 20 ambazo ni msaada wa fedha
kutoka serikali ya Mkoa wa Mbeya na baadhi ya wadau wa michezo ndani na
nje ya mkoa wa Mbeya.
''Tumekopa fedha kutoka kwa wadau
mbalimbali jumla ya Sh. milioni 13.5 zingine tumechangiwa na wadau na
wapenzi wa soka jumla tumetumia sh. milioni 22,326,000/-''alisema
Mwanjala.
Aliwataja waliokikopesha Chama Cha
Mipra wa Miguu mkoa wa Mbeya MREFA kuwa ni pamoja na Chama Cha Mpira wa
Miguu nchini TFF Sh. milioni 5, Halmashauri ya Jiji la Mbeya Sh. Milioni
5, Mnassi Communication Sh.Milioni 1.5, Barus General Interprises
Sh.milioni 2, na kufikia jumla ya Sh.milioni 13.5.
Mwanjala alisema kuwa fedha zingine
zimetokana na michango ya wadau mbalimbali wa soka na kwamba matarajio
uwanja huo utakamilika mapema kwa ajili ya mechi ya mzunguko wa pili
itakayoanza Januari 25 ambayo itawakutanisha maafande wawili kati ya
Timu mwenyeji Tanzania Prison ya Mbeya na Ruvu JKT ya Pwani.
NA RASHID MKWINDA
NA RASHID MKWINDA
No comments:
Post a Comment