Tuesday, January 7, 2014

WAFUASI WA ZITTO V/S CHADEMA MAHAKAMANI LEO

 Huyu mwenzake naye pia wa Chadema  akiwa na bango na kumfagilia Zitto
Wafuasi wa Chadsema wanaouunga mkono Zitto wakiwa wameunganisha mabango yao kuonyesha jina la Zitto mbele  ya mahakama kuu.


Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Z. Kabwe pamoja na Mwanasheria wake,Albert Msando (kulia) wakiwasili katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo huku wakiongozana na wafuasi wanaopinga kuvuliwa uongozi wake,tayari kwa kwenda kusikiliza kesi yake aliyoifungua dhidi ya Chama Chake cha CHADEMA inayosikilizwa leo Mahakama Kuu.
Wafuasi wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe wakimshangilia kiongozi wao alipokuwa akiwasili Mahakamani hapo leo.
Sehemu ya Wafuasi wa CHADEMA wasiomkubali Zitto Kabwe wakiwa na Mabango yao nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam


MIVUTANO YA KISIASA ISITUFIKISHE HAPA WATANZANIA

Wafuasi  wa  Chadema  wakizichapa baada ya  kuibuka mzozo  mahakamani kati ya Zitto Kabwe na Chadema ,hapa  kijana akilazimika kutimua mbio kunurusu uhai  wake
hapa  akiwa amekatwa mtama  wa  nguvu
Hapa  uzalendo wa  kutetea chama ama mtu ukiwa umemshinda
Kichapo  kikiendelea
Post a Comment