Sunday, February 9, 2014

HIZI SIASA UCHWARA;..CHADEMA WAJERUHI MBUNGE WA CCM MBEYA VIJIJINI

 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mch. Luckson Mwanjale.(Picha na maktaba ya kalulunga media).

SABA WAKAMATWA, WENGINE WASAKWA.

MBUNGE wa Mbeya Vijijini, Mchungaji Luckson Mwanjale, amejeruhiwa na vijana wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), alipokuwa eneo la Shipongo akifuatilia uchaguzi mdogo wa kata ya Santilya katika Jimbo hilo leo asubuhi.

Habari zinasema kuwa, Mwanjale alifika katika eneo hilo na kukuta uchaguzi unaendelea salama ingawa awali kulikuwa na rabsha za hapa na pale kati ya vijana wageni katika eneo hilo na vijana wa CCM wenyeji.

Vijana hao wageni, walipohojiwa kuwa walikuwa wakitafuta nini walidai kuwa wao ni mawakala wa Chadema ili hali mawakala wa chama hicho, walikuwa kwenye chumba ca uchaguzi.

Imeelezwa kuwa, vijana hao walitawanywa, kisha wakapigiana simu na wenzao ambao walienda umbali wa zaidi ya mita 300 kutoka kituo cha kupigia kura, ambako walimvizia Mbunge huyo na kumjeruhi vibaya kichwani na wakati wanataka kukimbia, vijana saba huku wengine wakifanikiwa kukimbia.

Mbali na Mbunge huyo, mwingine aliyejeruhiwa ni Mchumi wa CCM wilaya hiyo, aliyefahamika kwa jina la Mwanjuguja.

Baada ya hapo, gari moja lilishikiliwa na polisi huku lingine walilokuwa nalo vijana hao lilitolewa upepo eneo hilo.

Gari lililokuwa limetolewa upepo mpaka majira ya saa saba mchana huu likawepo eneo la tukio,  ni lenye namba za usajili T 222 AKG Toyota Hilux.

No comments: