Wednesday, February 26, 2014

JOSEPH MWAISANGO AFIKISHA MISAADA YA MAPACHA WANNE WAENDELEA KUKUA VIZURI, WASAMARIA WEMA WASHUKURIWA KWA MISAADA

Kibao kikionesha Kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba anakoishi mwanamke aliyejifungua mapacha wanne.

Msafara wa kuelekea Nyumbani kwa Mama wanne ukiwa unacha Lami barabara ya Sumbawanga Tunduma.


Baada ya kuwasili nyumbani kwa Mama Wanne, Moja ya wakurugenzi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango ambaye alikuwa ni kiongozi wa Msafara akionesha baadhi ya zawadi zilizopelekwa.

Baadhi ya watoto na wakazi wa kijiji cha Chiwanda wakisaidia kushusha  mizigo kwenye gari huku wakionesha kufurahia misaada hiyo.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha mpumpi kijiji cha Chiwanda, Winston Mtali akipokea msaada kwa niaba ya Familia kutoka kwa Joseph Mwaisango moja ya Wakurugenzi wa mbeya Yetu Blog kwa niaba ya Kampuni ya Michuzi Media waliofanikisha misaada hiyo kutoka Uingereza.

Erick Mwaisango akimkabidhi moja ya zawadi Mama Wanne kwa niaba ya Kampuni ya Nora SilverBoutique ya Jijini Dar Es Salaam.


Familia ya mama wanne ikiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya Wenyeviti wa Kijiji na kitongoji baada ya kupokea Msaada  kutoka kwa Wasamaria wema waliowakilishwa na Joseph na Erick Mwaisango.

Baba Wanne Webson Simkanga na mkewe Aida Nakawala wakiwa wamewabeba watoto wao.

Wanahabari Venance Matinya wa gazeti la Jamboleo na Ezekiel Kamanga wa Bomba fm Redio wakichukua maoni kutoka kwa Baba Wanne.


Mapacha wanne kutoka kulia ni Asifiwe, Daudi,Anania na Alinikumbu wakionesha nyuso za furaha ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa afya zao.

Baba na Mama wanne wakifurahia misaada iliyotolewa na wasamaria wema kwa ajili ya familia yao.WATOTO  wanne  waliozaliwa na mama mmoja kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya wanaendelea vizuri.
 Watoto hao walizaliwa na Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye amewashukuru wasamaria wema kwa kuendelea kuwapa misaada iliyosaidia watoto hao kukua vizuri.
Akizungumza na  www.mbeyayetu.blogspot.com  Nyumbani kwao jana Baba Mzazi wa watoto hao, Webson Simkanga(28) alisema yeye binafsi hana uwezo kiuchumi lakini kutokana misaada mbali mbali aipatayo kutoka kwa wasamaria wema inasaidia kuimarisha afya za watoto wake.
Alisema hivi sasa Watoto wake hao wamekua vizuri na kuleta matumaini kutokana na hali zao za kiafya na kuchangamka sana kinyume na matarajio ya watu wengi wasiokuwa na mapenzi mema kwa familia hiyo wakiombea mabaya kuwatokea.
Alisema kutokana na kuimarika kwa afya zao baba huyo ametoa majina kwa watoto wake hao huku akitarajia kuwabatiza kama ishara ya Wakristu ya kuwakabidhi watoto hao mikononi mwa Kanisa na Mungu.
Aliwataja majina watoto hao kuanzia wa kwanza hadi wa Mwisho kuwa ni Alinikumbu(mtoto  mwenye huruma), Daudi, Asifiwe na Anania ambao anatarajia kuwabatiza Machi 9, Mwaka huu katika kanisa la African Mission Church(AMC).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Chiwanda, Ignas Sinkara, alisema jukumu la kijiji bado lipo palepale kuhakikisha hali za watoto zinaendelea kuimarika siku hadi siku na kuongeza kuwa pia Wasamaria wema wanazidi kujitokeza kuwachangia familia hiyo.
Alisema mbali na wanakijiji kujitokeza kwa wingi kumsaidia mama wanne kubeba watoto na kusaidia kazi za nyumbani taasisi zingine bado zinatoa misaada yao likiwemo Kanisa Katoliki ambalo lilichangia Fedha tyaslimu Shilingi 56,000/= pamoja na Debe mbili za Mahindi na kusaidia kuandaa shamba la kupanda Mihogo la Familia hiyo.
Aidha katika Ziara ya Waandishi wa habari Kijijini hapo yenye lengo la kutaka kuwajulia hali watoto hao ikiwa ni pmoja na kuwasilisha  michango mbali mbali iliyotolewa na wasamaria wema kwa ajili ya familia hiyo.
Misaada hiyo ni pamoja na Msaada uliopokelewa ba Mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Jijini Dar Es Salaam wa www.michuzi.blogspot.com ulipokea kutoka kwa Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ambaye alitoa maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto.
Msamaria  mwema mwingine aliyejulikana kwa Norah SilverBoutique toka DSM ambaye ametoa Maziwa Lactogen Dazan Mbili yaani makopo 24 pamoja na nguo vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Laki Tano.
Pia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini iliwezesha usafiri kwa wanahabari hao kwa kuchangia Mafuta, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza na ofisi za Michuzi Media Group (MMG) kuwezesha  kufika kwa mizigo hiyo Jijini Mbeya.
Na Mbeya yetu
Post a Comment