Sunday, February 16, 2014

MAPATO kwa mechi ya ligi ya Vodacom kati ya timu za Mbeya City ya Jijini Mbeya na Simba ya Jijini Dar es salaam yamevunja rekodi zapatikana shilingi Milion 105

Katika mechi hiyo ya jana ambayo timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1.



Vijana wakijitoa  muhanga katika mechi ya mbeya city na simba baada ya kukosa tiketi ya kuingia uwanjani



Afisa habari wa timu ya Mbeya City Freddy Jackson akiwa na tiketi zisizopigwa mhuri na kusema kuwa tiketi hizo zimeghushiwa kwa nia ya kuhujumu mapato ya mchezo huo.

Imani za kishirikina zilikuwepo uwanjani hapo  hebu ona huyo jamaa suruali imeloa kitu kama mafuta aliyoweka mfukoni kupasuka





Simba ya Jijini Dar es salaam 

Mbeya City 












Katika Mchezo huo jumla ya tiketi 21,000 ziliuzwa na kumalizika na kuingiza mapato jumla ya sh. milioni 105.
Katika mapato hayo kila timu ilipata kitita cha sh. milioni 25.3 ambapo sh.milioni 12.8 zilibaki kwa ajili ya uwanja,sh.milioni 7.7 kwa ajili ya maandalizi na sh. milioni 7.7 kwa ajili ya kamati ya ligi ilhali sh. milioni 3.8 zilikuwa ni kwa ajili ya chama cha mpira wa miguu TFF.

picha na Mbeya yetu

No comments: