Sunday, February 16, 2014

MKUU WA WIALAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AONGOZA SKAUTI WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA SIKU YA KUFUNGA KAMPENI YA UPANDAJI MITI MASHULENI NA KATIKA VYANZO VYA MAJI NA UFUGAJI WA NYUKI

MWENYE KOFIA NI MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIWA NA VIJANA WAZALENDO WA SKAUTI WILAYA YA RUNGWE HAPA NI BAADA YA MAPOKEZI NA KUELEKEA SEHEMU YA TUKIO LA KUPANDA MITI ZOEZI LILIOFANYIKA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA MASOKO

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE AKIVISHWA SKAFU YA HESHIMA NA KUTAMBUA KUWA MKUU WA WILAYA NI MLEZI NA MSHAURI MKUU WA SKAUTI WILAYA

GWALIDE LA SKAUTI WILAYA YA RUNGWE  IKIWA NI MAPOKEZI YA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE NA BARAZA LA SKAUTI WILAYA YA RUNGWE WALIOFIKA KUONA KAMBI LA VIJANA WA SKAUTI WILAYA YA RUNGWE AMBAPO KAMBI IMEFANYIKA KWA SIKU TATU KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA MASOKO

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN AKIJIONEA MMOJA WA SKAUTI WILAYA YA RUNGWE AKIONYESHA JINSI YA KUPANDA MTI WA MPARACHICHI AMBAPO KATIKA KAMBI HILI LA SIKU TATU VIJANA WA SKAUTI WAMEFUNDISHWA MAMBO MBALIMBALI IKIWA PIA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI, UTII NA UZALENDO PAMOJA NA UKAKAMAVU

MKUU WA WILAYA AKIPANDA MTI MTI WA MPARACHICHI IKIWA NDIO ISHARA YA SIKU YA KILELE CHA KUPANDA MITI WILAYA YA RUNGWE AMBAPO ZOEZI LA KUPANDA MITI LILIANZA TAREHE 12.01.2014 NA LEO NDIO SIKU YA KILILE, KATIKA ZOEZI HILI SHULE NA TAASISI AMBAZO SKAUTI WAPO WAMESHIRIKI KUPANDA MITI IPATAYO 4200 KWA MWAKA 2014 TU IKIWA NI MWAKA WA SITA TANGU KUANZISHWA KWA UTARATIBU HUU WWA HALMASHAURI YA RUNGWE KUWASHIRIKISHA SKAUTI KUTUNZA MAZINGIRA NA KUSIMAMIA SEHEMU ZA VYANZO VYA MAJI

KUANZIA KUSHOTO NI ENZI SEME AMBAYE NI AFISA MICHEZO WA WILAYA YA RUNGWE, KATIKATI NI PETER CHIBWAYE AMAYE NI AFISA MALIASIRI WILAYA YA RUNGWE NA KULIA NI MAKINGO SHIJA AMBAYE NI MKUU WA SHULE YA MASOMO AMBAPO KAMBI LA SKAUTI LIMEFANYIKA KWA SIKU TATU NA VIJANA WAMEJIFUNZA MAMBO MBALIMBALI PAMOJA NA KUPANDA MITI AINA MBALIMBALI 1500.


KAMISHINA WA SKAUTI WILAYA YA RUNGWE JAROME JERICO AKITAMBULISHA VIONGOZI WENZAKE NA KUELEZA MIKAKATI YA SKAUTI WILAYA YA RUNGWE MASHULENI MWAO NA KATIKA SHUGHURI ZA KIJAMII
MAFUNZO YA SKAUTI YANAFANYIKA KWA KUZINGATIA UMLI WA MTOTO NA WATOTO HUFUNDISHWA UKAKAMAVU, UTII NA UZALENDO KWA NCHI YAO YA TANZANIA PIA SKAUTI NDIO MTU WA ULINZI WA AMANI SEHEMU ANAYOISHI

MWENYEKITI WA BARAZA LA SKAUTI MR SANGA AKIONGEA NA VIJA WA SKAUTI HAWAPO PICHANI NA ZAIDI AMEWAPONGEZA SANA VIJANA KWA KUJITOLEA KWA HALI NA MALI NA KUWA WATOTO MAJASIRI KUKAA NA KUFANYA KAZI ZA KIJAMII,

MTUNZA HAZINA WA BARAZA LA SKAUT WILAYA YA RUNGWE JULIANA NANKOMA AMBAYE NI HAKIMU MFAWIDHI WA WILAYA YA RUNGWE AKIONGEA NA VIJANA WA SKAUTIAMESEMA VIJANA KUPENDA USKAUTI NI KUKIJENGEA KUWA KIJANA MKAKAMAVU NA MAZALENDO KWA NCHIYAKO NA KUWA TEGEMEO LA TAIFA

AFISA MICHEZO WA WILAYA YA RUNGWE ENZI SEME AMEWATALKA VIJANA KUZINGATIA MAFUNZO WANAYOPEWA NA VIONGOZI WAO KWA KUWA NI  FAIDA KWA TAIFA HIVYO TAIFA LITAKUWA NA VIJANA WAADILIFU NA WAZALENDO KWA KUFANYA KAZI ZA KIJAMII NA KUJITOLEA HASA ZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

NAIBU KAMISHINA WA SKAUTI WILAYA YA RUNGWE PETER KIBONA AKISOMA RISALA KWA MGENI RASIM AMBAPO AMEELEZA MIKAKATI YA SKAUTI WILAYA YA RUNGWE KUWA NI KUJENGA UMOJA NA NIDHAMU KWA VIJANA MASHULENI, KUSIMAMIA MAZINGIRA KATIKA MAENEO YAO, PIA AMEWATAKA BAADHI YA WAKUU WA SHULE KUWA NA MWITIKIO WA KUANZISHA SKAUTI NA KUSAIDIA VIJANA WANAPOTAKIWA KUFIKA KATIKA KAMBI LA SKAUTI KWAKUWA VIJANA HUFUNDISHWA MAMBO MBALIMBALI HASA YA KIJAMII KAMA KAMBI HILI VIJANA WAMEPATA MAFUNZO YA KUPANDA MITI YA MAPARACHICHI YA KISASA HIVYO VIJANA KWENDA MASHULENI MWAO KWA KUSHIRIKIANA NA WALIMU WAO KUANZIHSA MASHAMBA YA MITI YA MAPARACHICHI IKIWA NI MRADI WA SHULE

PETER CHIBWAYE AMEELEZA MIKAKATI YA WILAYA KWA KUWATUMIA SKAUTI KUTUNZA MAZINGIRA AMBAPO AMESEMA WILAYA YA RUNGWE IMEPITISHA UANZISHWAJI WA MIZINGA YA NYUKI KATIKA VYANZO VYA MAJIAMBAPO AMESEMA MIRADI HUU WA UFUGAJI WA NYUKI UTABORESHA SANA UTUNZAJI WA MAZINGIRA HASA KATIKA VYANZO VYA MAJI PIA AMESEMA KUWA HADI KWA MWAKA 2013/2014 HADI MWEZI HUU MITI 698,314 IMEPANDWA WILAYANI RUNGWE NA KWA TAKWIMU ZA TANGU MWAKA 2008 HADI MWAKA HUU MITI 8,141, 418 MITI IMEPANDWA HIVYO KWA KASI HII ANGALAU MAZINGIRA YAMEANZA KURUDI KATIKA KAMA ZAMANI HIVYO AMEWATAKA VIJANA KUJITOLEA KUTUNZA SANA MAZINGIRA HASA KATIKA VYANZO VYA MAJI.

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE AKIONGEA NA VIJANA WA SKAUTI NA VIONGOZI WAO AMEWATAKA VIJANA KUJIFUNZA UADILFU NA KUWA WAZALENDO KWA TANZANIA YAO PIA AMESEMA KUWA NAFASI ZA KUJIUNGA NA  MAJESHI YA TANZANIA AMBAZO ZINAOMBWA NA WATU MBALIMBALI KUANZIA WILAYA ZAO SASA SERIKALI IMEANZA KUANGALIA NA KIGEZO CHA KIJANA ALIVYOKUWA ANAJIHUSISHA NA UMOJA  WA SKAUTI NA TAKUKULU KATIKA MASHULE YAO KWAKUWA VIJANA WANAOJIHUSISHA NA VIKUNDI HIVI WANAJIFUNZA UKAKAMAVU, UZALENDO NA HASA KUJITOLEA KWA HALI NA MALI HIVYO AMEWATAKA WAZAZI NA WALIMU KUJITOLEA ILI KUWAWEZESHA VIJANA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA MAKAMBI KAMA HAYA YA SKAUTI, KUTOKANA NA MAFUNZO HAYA YA SKAUTI.  MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AMESEMA ILI KUONGEZA MIRADI MASHULEN WANAFUNZI WALIOSHIRIKI KAMBI HILI NA KUJIFUNZA JINSI YA KUANZISHA MASHAMBA YA MITI YA MAPARACHICHI KWENDA MASHULENI KWAO NA KUANZA KUPANDA MTI MOJA MOJA KWA KILA MWEZI WA MWAKA HUU HIVYO KUFIKIA MWEZI WA KUMI NA MBILI KILA MWANAFUNZI ANATAKIWA KUWA NA MITI KUMI NA ZOEZI HILI ATALISIMAMIA MWENYEWE KWA KUTEMBELEA KILA SHULE KUONA SKAUTI WAMEFANYA NINI

MMOJA WA VIJANA WA SKAUTI AKAPATA WASAA WA KUSHUKURU JUHUDI ZA SERIKALI KUIMARISHA SKAUTI MASHULENI KWAKUWA IMEONGEZA SANA UADIRIFU NA USIMAMIZI WA LASLIMALI ZA MASHULE KWAKUWA SKAUTI NI KIONGOZI NA MSIMAMIZI WA MANI KATIKA ENEO ANAPOISHI HIVYO AMEMTAKA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE NA BARAZA LA SKAUTI KUENDELEA KUANDAA MAKAMBI ILI VIJANA KUENDELEA KUJIFUNZA

HAKUNA LEGELEGE HAPA KILA HATUA NI UKAKAMAVU

VIJANA WA SKAUTI WAKIWEKA ULINZI KUHAKIKISHA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE NA WAJUMBE WAKE WANAONDOKA WAKIWA SALAMA KATIKA SHULE YA MASOKO AMBAPO KAMBI YA SKAUTI IMEFANYIKA NA KUWAKUSANYA VIJANA WA SKAUTI KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI WILAYANI RUNGWE

No comments: