Wachezaji wa Mbeya City wakipanda
ndege mchana jana Uwanja wa Ndege wa Songwe mkoani Mbeya kuelekea
Mombasa, Kenya ambako watakaa hadi Jumamosi asubuhi watakapokwenda Tanga
na jioni yake kucheza mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi
ya wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani.
......................................................
Mbeya City waanza mchakato wa ujenzi wa uwanja wao
TIMU ya Mbeya City ya Mbeya, ipo
kwenye mchakato wa ujenzi wa uwanja wao na kushusha nchini kontena moja
la jezi zao kutoka nchini China.
Mbeya City iliyopanda daraja msimu
huu, kama ikifanikiwa kutimiza yote hayo basi kimaendeleao itazizidi
klabu kongwe za Simba na Yanga ambazo hadi sasa hazina hata viwanja vya
maana vya mazoezi.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Mussa Mapunda
anasema kuwa tayari wamenunua shamba la ekari 15 eneo la Iwambi, Mbeya
ambalo wamelitenga kwa ajili ya kujenga uwanja mkubwa wa kisasa.
Anasema, tofauti na uwanja wamepanga
kujenga hosteli za kisasa watakazozitumia wachezaji wa timu kubwa, pia
kwa ajili ya timu zao za vijana kuanzia umri chini ya miaka 14 hadi 20
watakaowatumia siku zijazo.
Pia watatenga eneo lingine kwenye
uwanja huo kwa ajili ya kituo cha michezo. Timu hiyo kwa sasa inatumia
Uwanja wa Sokoine unaomilikiwa na CCM.
Akifafanua kuhusu kuingiza nchini
kontena moja la vifaa vya michezo kutoka China ambalo litakuwa na jezi,
suti za michezo, kofia, skafu, bendera na soksi. Vitu hivyo vitauzwa
nchini kote pamoja na nchi za Malawi na Zambia. ......................................................
No comments:
Post a Comment