Thursday, February 20, 2014

MKUTANO MKUU WA WAKULIMA WADOGO WA CHAI WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA NA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI WA KIDEMOKRASIA KUCHAGUA VIONGOZI WA WAKULIMA WADOGO WA ZAO LA CHAI WILAYA NI RUNGWE WATAKAO KAA MADARAKANI KWA MUDA WA MIAKA MITANO

MWENYEKITI WA WAKULIMA WADOGO WA CHAI WILAYANI RUNGWE JONSON MWAKASEGE AKIFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA KIKATIBA WA WAKULIMA WA CHAI MKUTANO AMBAO UNAWAJUMUISHA WAJUMBE WA SKIMU TISA ZA WAKULIMA WA CHAI ELFU KUMI NA TANO WANAOMILIKI HISA KATIKA KIWANDA CHA CHAI CHA  WAKULIMA WATCO KATUMBA WILAYA YA RUNGWE. AMBAPO KATIKA MKUTANO HUU WZA MWAKA  HUJADILI MAMBO MBALIMBALI YA UMOJA IKIWEPO AJENDA YA UCHAGUZI KWA KUWA MWAKA HUU NI MWAKA WA KIDEMOKRASIA YA UCHAGUZI WA UCHAGUZI KWA KUCHAGUA VIONGOZI WA KUONGOZA UMOJA WA WAKULIMA WA CHAI WILAYA YA RUNGWE KWA MUDA WA MIAKA MITANO MINGINE

WAJUMBE WA MKUTANO WAKIWA KATIKA VIWANJA VYA OFISI YA YA WAKULIMA WADOGO WA CHAI WILAYA YA RUNGWE RSTGA  ILIYOPO TUKUYU MJINI WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA WAKIWA KATIKA MKUTANO MKUU WA MWAKA CHA WAKULIMA WA CHAI WILAYANI RUNGWE

MGENI RASMI KATIKA MKUTANO MKUU WA WAKULIMA WA CHAI WILAYANI RUNGWE MKUU  WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AMEWATAKA WAKULIMA KUENDELEA KUWA NA USHIRIKIANO WA KUKAA NDANI YA UMOJA WAO KWAKUWA KUNA FULSA KUBWA SANA, PIA AMEWATAKA WAKULIMA KUONGEZA UZALISHAJI WA ZAO LA CHAI KWA KUYAENDELEZA MASHAMBA YALIYOTELEKEZWA NA KUANZISHA MASHAMBA MAPYA YA CHAI, PIA AMEITAKA BODI YA CHAI NA WADAU KUANZISHA MKAKATI WA KUWAENDELEZA WAKULIMA KWA KUPATA MKOPO WA KUJENGA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU KWA WAKULIMA AMBAPO AMESEMA KUWA TAASISI YA KIBENKI YA CRDB TAYARI IKO TAYARI KUANZISHA  MPANGO HUO WA KUWAWEZESHA WAKULIMA KUPATA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU ILI KUFANYA MKULIMA KUISHI KATIKA NYUMBA NZURI INAYOENDANA NA UZURI WA ZAO LA CHAI AMBALO NDIO ZAO TEGEMEWA KATIKA UCHUMI WA WANANCHI WA WILAYA YA RUNGWE

MTENDAJI MKUU (CEO) WA RSTGA LEBI G. MWAKATOBE AKITOA MWONGOZO WA UCHAGUZI WA KUMCHAGUA MWENYEKITI WA RSTGA, MAKAMU WAKE NA WAJUMBE WANAWAKE WATAKAOINGIA KATIKA BODI YA RSTGA ILI KUWEKA USAWA WA KIJINSIA
BODI YA WAKULIMA WA CHAI WILAYANI RUNGWE RSTGA ILIYOFANYA KAZI KWA MUDA WA MIAKA MITANO UKAFIKA MUDA WA KUJIUZURU ILI KUPISHA UCHAGUZI HURU ILI WAJUMBE WAPIGE KULA KUPATA  KIONGOZI  MWENYEKITI WA  WAKULIMA WADOGO WILAYANI RUNGWE UMOJA RSTGA AMBAO UNAUBIA WA KUENDESHA KUWANDA CHA CHAI CHA WATCO CHA KATUMBA NA MWAKALELI

UPIGAJI KULA UKAENDELEA KWA WAJUMBE  MKUTANO MKUU WA RSTGA 2014

MUDA WA KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI UKAFIKA

WAJUMBE NA VIONGOZI WA WATCO KATUMBA WAKIWA MAKINI KATIKA KUSIKILIZA NA KUANGALIA UCHAGUZI UNAVYOENDESHWA

WAPILI KULIA MSTALI WA MBELE NI JOHNSON MWAKASEGE AMBAYE AMECHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA WAKULIMA WA CHAI  WILAYANI RUNGWE NA WENGINE NI WAJUMBE WA BODI YA WAKULIMA WA CHAI AMBAO WANATOKANA NA KUCHAGULIWA KWENYE SKIMU ZAO VIJIJINI AMBAPO WILAYA YA RUNGWE INAUNDWA NA SKIMU TISA ZA UZALISHAJI WA CHAI

WAJUMBE WA MFUKO WA MAENDELEO WA RSTGA

UCHAGUZI UMEFANYIKA KWA WANAWAKE WATATU KUINGIA KATIKA BODI YA RSTGA NA WAWILI KUINGIA KATIKA BODI YA MFUKO WA MAENDELEO ILI KUWEKA USAWA WA WANAWAKE NA WANAUME KATIKA VIKAO VYA MAAMUZI VYA WAKULIMA WA CHAI WILAYANI RUNGWE

BAADA YA KUISHA KWA AJENDA YA UCHAGUZI WAJUMBE WAKAPATA WASAA WA KUPITIA NA KUANGALIA YALIYOTEKELEZWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO NA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA PIA WAJUMBE WAKAPATA WASAA WA KUULIZA MASWALI NA KUTOA MAONI YA KUENDELEZA UMOJA WA WAKULIMA WA CHAI WILAYANI RUNGWE HUKU CHANGAMOTO IKIWA NI UPATIKANAJI WA PEMBEJEO NA HASA MBOLEA PIA WAKULIMA KUUZA CHAI NJE YA UMOJA WAO KATIKA KIWANDA CHA CHAI MOHAMMED - MSEKELA

MTAALAMU WA KILIMO NA UTAFITI MR MHAGAMA WA WATCO AKITOA MAELEZO YA KINA KWA WAJUMBE JINSI SOKO LA CHAI LINAVYOYUMBA KATIKA SOKO LA DUNIA PIA MHAGAMA AMESEMA KUWA WAKULIMA KUKAA NDANI YA UMOJA KUNA FAIDA KUBWA SANA KWANI KUENDESHA VIWANDA VIWILI KWA UZALISHAJI NI GHARAMA  HIVYO WAKULIMA WANATAKIWA KUUZA MAJANI MABICHI YA CHAI KATIKA KIWANDA CHAO CHA KATUMBA NA MWAKALELI

KULIA NI JUMA LIGANJA MTUNZA HAZINA MKUU WA RSTGA AKIWASILISHA TAARIFA YA FEDHA KWA WAJUMBE WA MKUTANO YA MWAKA 2013 NA TAARIFA YA FEDHA YA MAKISIO YA MWAKA 2014 AMBAPO MPAKA SASA JUMA AMESEMA KUWA MAHESABU YA UMOJA KWA UKAGUZI WA MKAGUZI WA NDANI NA NJEMA HESABU YAMEPATA HATI SAFI


WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WAKIHAILISHIWA MKUTANO
MAKAMU MWENYEKITI WA RSTGA JACKSON MWAMPULULE AKIFUNGA MKUTANO MKUU WA MWAKA 2014 AMEWATAKA WAJUMBE WOTE WANAO WAWAKILISHA WAKULIMA WA CHAI VIJIJINI KUWA WAJUMBE WAZURI KWA YALE YOTE YALIYO AZIMIWA KWA AJILI YA UTEKELEZAJI KWA MWAKA 2014 PIA AMEWATAKA WAJUMBE KUWA MFANO WA UZALISHAJI WA CHAI ILI KUONGEZA
KINGOTANZANIA - 0752881456

No comments: