Saturday, February 1, 2014

MWENYEKITI WA CCM DR. JAKAYA KIKWETE AWASILI MKOANI MBEYA TAYARI KWA SHEREHE YA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM

1Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akishuka kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya mara baada ya kuwasili rasmi mkoani humo tayari kwa kuongoza maadhimisho ya Miaka 37 ya Chama cha Mapinduzi yanayofanyika kesho kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ambapo amepokelewa na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa Chama na Serikali pamoja na wananchi waliojitokeza katika mapokezi hayo. 2Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Songwe. 3Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abas Kandoro na Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman Sigalla kushoto. 4Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Marck Mwandosya Waziri asiyekuwa na Wizara maalum, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla na kushoto ni Dr. Harrison Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi. 5Mwenyekiti wa Cma Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Kamnda wa Polisi mkoa wa Mbeya SACP AHMED Z. MSANGI . 7Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr.Jakaya Kikwete akipokea heshima kutoka kwa kikosi cha vijana wa Chipukizi mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Songwe kulia ni  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi na kutoka kushoto ni  Dr. Harrison Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abas Kandoro, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman Sigalla na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana 8Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr.Jakaya Kikwete akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili mkoani humo kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM  11Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na  viongozi na wabunge 12Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na vijana wa UVCCM. 13 14Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa katika kikao cha ndani na viongozi wa CCM mkoa wa Mbeya kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti Bara na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi 15 
Wajumbe wa halmashauri kuu mkoa wa Mbeya wakiwa katika kikao hicho. 
 17 
Ndege ya Rais Jakaya Kikwete ikiwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya

KINGOTANZANIA - 0752881456
Post a Comment