Saturday, February 1, 2014

SUPPORT FOR MISS TANZANIA 2013 HAPPINESS WATIMANYWA

Hey
guys. At Miss World, contestants usually need as much support as they
can get. I would therefore like to ask for your help in spreading the
word to your fellow fans, friends, family, acquaintances etc. about the
representative for Tanzania this year;
Happiness Watimanywa.
People around the world can help me make an even bigger impact through social media and I would like you to be informed of my journey from as early as now.

Please follow:
@misstanzania2013 on Instagram
@misstz2013 on twitter
And Like Miss World-Tanzania on Facebook
Thanks for the support.
Happy

..........................................................................


wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati na Madini watembelea na kukagua miradi inayotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini mkoani Mwanza
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo  akitoa ripoti fupi mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati na Madini juu ya miradi inayotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini  walipomtembelea ofisini kwake ili kuelezea nia yao ya kufanya ziara katika mkoa huo.
..........................................................................

Muhongo: Hatudanganyiki tena na wawekezaji madini

Madini1 d6791
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospiter Muhongo, amejigamba kuwa Tanzania haitadanganyika tena kwa wawekezaji wa sekta ya madini kutolipa kodi na kuifanya nchi kutofaidika na rasilimali zake

Alisema hayo baada ya Serikali za Tanzania na Finland, kutiliana saini, makubaliano katika kutafiti na kukuza sekta ya madini.

"Kama ni kutuibia walifanya hivyo siku za nyuma, lakini kwa sasa hawawezi tena," alijigamba Profesa Muhongo akidai historia inaonyesha kuwa nchi zote zenye rasilimali za madini, mwanzoni zilidanganyika.

Alikiri kuwa awali wawekezaji katika migodi walikuwa wakijitetea kuwa walikuwa wanapata hasara lakini kwa sasa, sheria inawalazimisha kulipa asilimia 30.
Kauli ya Profesa Muhongo ilitokana na waandishi kumbana, kuhusu Watanzania kutonufaika na sekta ya madini wakati ina faida kubwa.

Profesa Muhongo alisema kwa sasa sekta ya madini inachangia asilimia 3.5 ya pato la Taifa.
Alisema malengo ni kuhakikisha kuwa sekta ya madini inachangia zaidi ya asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

Mapema, wakurugenzi wa sekta ya madini katika Serikali za Tanzania na Finland, walitiliana saini ya kukuza na kuendeleza sekta ya madini hapa nchini.
Akizungumzia makubaliano hayo, Profesa Muhongo alisema yanazingatia mambo matatu, ambayo ni pamoja na utafiti wa madini katika mikoa ya kusini.

Alisema kimsingi tayari wamegundua kuwa ukanda huo una makaa ya mawe, shaba, niko na platiniamu.
Alisema watakachokifanya ni kuainisha maeneo yenye madini na viwango halisi ili wakipatikana wawekezaji wa kuyachimba, waingie kwenye makubaliano ya uhakika. 

Chanzo: Mwananchi

No comments: