ILIKUWA mwezi, wiki, siku, masaa na
sasa limetimia ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika
uchaguzi wa kumpata Mbunge wa jimbo la Kalenga, baada ya kuzoa kura kwa
asilimia 79.4 dhidi ya wapinzani wao Chadema waliopata asilimia 20.1 na
Chausta 0.51.
Kwa nafasi hiyo, Mgombea wa CCM
Godfrey Mgimwa amekuwa Mbunge mpya akichukua nafasi ya Mbunge
aliyefariki jimboni humo, Dr William Mgimwa.
Matokeo ya uchaguzi huo, yanatoa
nafasi nyingine kwa CCM kuweka rekodi ya kushinda chaguzi ndogo za
ubunge katika majimbo mbalimbali yaliyokuwa nyameachwa wazi.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, CCM imeshinda kwa kura 22,943 dhidi ya kura 5,800 za Chadema huku chausta ikiambukia 143.
Ushindi wa jimbo la Kalenga, ni mwanzo wa kuanza mbio nyingine za uchaguzi katika jimbo la Chalinze.
Mbunge mteule wa jimbo la Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa
akibebwa juu na wanachama wa CCM huku wakiserebuka kusherekea ushindi
katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa Iringa ambapo CCM imeshinda kwa mbali
katika matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye jimbo la
Kalenga mkoni Iringa, Tume ya taifa ya uchaguzi imemtangaza Godfrey
Mgimwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo ambapo CCM imeshinda kwa kura
22962 huku CHADEMA ikipata 5853 na chama cha CHAUSTA kura 150 Chama cha
Mapinduzi kimefanikiwa kushinda katika kata zote kumi na tatu za jimbo
hilo.
MATOKEO KAMILI HAYA HAPA
No comments:
Post a Comment