Saturday, March 8, 2014

MBEYA CITY YAICHAPA RHINO 3-1 UWANJA WA SOKOINE MBEYAIMG-20131029-WA0076 
Vijana wa kocha Juma Mwambusi wamewabamiza Rhino Rangers 3-1. Wasema safari yao bado inaendelea.
WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya maafande wa Rhino Rangers katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara ndani ya dimba lao la Sokoine jijini Mbeya.
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na said Kipanga aliyefunga mawili , huku la tatu likitiwa kimiani na Deus Kaseke.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, afisa habari wa Mbeya City, Fredy Jackson  amesema kuwa mchezo ulikuwa mgumu sana kwani Rhino waliingia uwanjani kwa lengo la kutafuta pointi tatu.
“Rhino wameonesha upinzani mkubwa sana katika mchezo wa leo. Walidhamiria sana kupata ushindi, lakini ubora wa wachezaji wetu umetusaidia”. Alisema Fredy.
Post a Comment