Naibu Waziri wa Fedha mhe Mwigulu Nchemba amehutubia kikao cha
pamoja cha bunge la ACP na EU katika mji wa Strasbourg nchini Ufaransa.
Katika hotuba yake, mhe Mwigulu
alianza kwa kukishukuru chombo hicho kwa ajili ya msimamo wake usioyumba kwenye
maswala ya amani akitolea mfano wa kazi nzuri waliofanya kwenye swala la
Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudani
Kusini. Mhe Mwigulu aliitaka Jumuiya ya Kimataifa imsaidie Rais wa muda
Mama Carthrine Samba Panza ili kuwezesha kipindi cha mpito na maridhiano
kuwezesha zoezi la uchaguzi huru na wa haki.
Kuhusu maswala ya kiuchumi mhe
Mwigulu aliwakumbusha wajumbe wa bunge hilo
kuwa umebaki mwaka mmoja tu kumalizia mpango wa malengo ya Maendeleo ya
Milenia (MDG’s). Mhe Mwigulu aliitaka
Jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kuwa mpango wa maendeleo baada ya 2015
unalenga nguzo tatu mhimu akizitaja
kuwa kijamii, kiuchumi na
Mazingira.
Kuhusu kiuchumi na Kijamii
mhe Mwigulu alisema kuna umhimu sasa wa kuhakikisha malengo yanalenga sector
zinazogusa na kubadilisha maisha ya watu wachini na masikini. ‘Tumekuwa na
kipindi cha kutosha kushughulikia uchumi mkubwa , tumefanikiwa sana, ila maeneo
mengi sekta zilizokuwa hazigusi maisha ya mtu masikini na hazitengenezi ajira
kwa watu masikini’ hivyo malengo
yamekuza uchumi na kuongeza pengo kati ya watu masikini na watu matajiri.
Ni
kiu yangu kuona agenda ya baada ya 2015 inalenga kuwainua masikini kwa kulenga
sekta zinazogusa maisha ya watu masikini na kutengeneza na kubooresha fursa
kwenye sekta zinazogusa watu wengi. Umhimu huo pia utolewe kwenye swala la
mazingira kwani mazingira yanaathiri zaidi shughuli za mtu wa hali ya chini.
Mhe Mwigulu alisisitiza kuwa kuna
uhitaji mkubwa zaidi wa kuendeleza sekta binfsi kwa kutengeneza sekta binfsi
inayolenga ujasiliamali zaidi na kutengeneza elimu ya kujiajri. Kwa sasa
misaada mingi inalenga elimu ya siasa na haki za binadam. “Elimu nzuri zaidi ni
ya kujiajiri na haki mhimu zaidi ni ya
kuishitena maisha bora” kama tunasaidia kuelimisha uraiani tusaidie kulimisha
ujasiliamali, ubunifu wa miradi, uendelezaji miradi, biashara na kutambua fursa.
Misaada ilenge kutambua fursa za uzalishaji, kuwekeza kwenye sekta za
uzalishaji na kutambua masoko. Mhe Mwigulu alisema, soko la Ulaya limekuwa
likiathiri sana mazao ya Afrika kwa bei kutokutabirika na bei kuyumba sana.
Mafia makubwa yanalinda wakulima wao na yanazuia mataifa madogo kulinda
wakulima wao.
Mataifa makubwa yanalinda mazao ya wakulima wao kwa
kuwahakikishia masoko lakini yanawapambanisha na wakulima wa mataifa madogo wasiokuwa na
ruzuku ya kutosha na wanaopangiwa bei za chini kwa mazao yao. Tukiamua kuinua
maisha ya mkulima masikini wa Afrika, tufute wimbo wa kushuka kwa bei za mazao
yake ktk soko la Dunia huku wakulima wa
mataifa makubwa wakiwa wamepata hifadhi.
Katika hatua nyingine Mwigulu
aliitaka Jumuiya ya kimataifa kufikia mwisho kwenye Economic Partnership
Agreements kwa kanda ambazo hazijakamilisha kwani limekuwa jambo la muda mrefu.
Wanajua kinachokwamisha, wafike mahali wayasikilize na matakwa ya mataifa
madogo kama kweli lengo la makubaliano na nia ni kuyanufaisha mataifa madogo
ili yaendelee. Alitambua kuwa Afrika Magharibi wamepiga hatua, lakini kwa EAC
na SADC mnatambua mahitaji yetu, tusikilizeni. “there can be no celebration in reaching a deal for the sake of it and
thereafter, encounter problems with its implementation”. Serikali zitapoteza
mapato kutokana na kupungua au kuondolewa kwa tarrifs kuathiri sana
utoaji wa huduma kwa jamii, hivyo nivyema tukajua hizi Economic Partnership Agreements
zinachangia vipi kuyafikia Malengo ya Milenia.
Baada ya hotuba hiyo ya dakika 15
ulikuja wakati wa maswali ya papo kwa papo ya dakika 15 ambayo wajumbe wa ACP –EU
waliuliza maswali na alijibu kwa ufasha kama
No comments:
Post a Comment