Thursday, March 20, 2014

CCM ILIVYOZINDUA KAMPENI ZAKE KWA KISHINDO JIMBO LA CHALINZE

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakipunga mikono baada ya kuwsili kwenye Uwanja wa Miembe saba, kwa ajili ya mkutano wa kufungua kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
 Wananchi wakimshangilia Ridhiwani baada ya kuwasili kwenye Uwanja huo

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCm katika uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete katika uzinduzi wa kampeni za CCM kuwania jimbo hilo leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kuzindua kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Miembe saba, Chalinze mkoa wa Pwani.
  Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiomba kura wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kuzindua kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Miembe saba, Chalinze mkoa wa Pwani.
 Mjumbe wa NEC ya CCM kutoka wilaya ya Lindi, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) akiwa na wananchi wengine kumshangilia mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCm katika jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa kufungua kampeni za CCM uliofanyika leo
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa mkutano huo wa kampeni
 Ridhiwani akidhihirisha furaha yake baada ya mkutano wake wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze kufiurika watu leo. Wengine kulia ni Mama Salma Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
 "PANDA KAKA UFANYE MAMBO" Inaelekea ndivyo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alikuwa akisema wakati akimsaidia Ridhiwani kupanda jukwaa la wasanii wakati wa mkutano huo.
 Nape na Ridhiwani wakiselebuka wakati wa burudani iliyotolewa na msanii Linex  jukwaani
 Ridhiwani akiwapungia mkono wananchi baada ya kuselebuka jukwaani
 Ridhiwani akiwaaga mashabiki kabla ya kushuka jukwaa la wasanii
 Nape akimsaidia Ridhiwani kushuka toka jukwaani
 Mbunge wa simanjiro Ole Sendeka akimuo9mbea kura Ridhiwani
 Khadija Kopa akitumbuiza na kundi zima la TOT wakati wa mkutabo huo wa kampeni
 Meneja wa kampeni za kumnadi Ridhiwani kuwania Ubunge wa Chalize, Mzee Kazidi akieleza kwa uchache sifa za Ridhiwani.,
Nape akimsikiliza kwa makini Khadija Kopa wakati akiambiwa jambo wakati wa mkutnao huo wa kampeni
 
 Mmoja wa kina mama walioonyesha kuhamasika kwenda kwenye mkutano huo, akiwa na bango la Ridhiwani  huku amebeba mtoto wake wakato akienda kwen ye mkutano huo
Meza kuu. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog
Post a Comment