Friday, March 21, 2014

DAKIKA 155:46 ZA HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salama ya heshima kutoka Jeshi la Polisi kabla ya hotuba ya uzinduzi wa Bunge maalum la Katiba leo mjini Dodoma.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride liliandaliwa na Jeshi la Polisi kabla ya hotuba ya uzinduzi wa Bunge maalum la Katiba leo mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta (kulia) na Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu wakijadiliana jambo nje ya ukumbi wa Bunge kabla hotuba ya uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutuba Bunge Maalum la Katiba wakati wa sherehe za uzinduzi wa Bunge hilo leo mjini Dodoma.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Mh. Seif Sharif Hamad (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu(Katikati) na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Amaan Abeid Karume Wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Hotuba ya Uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma Leo.


 Rais Jakaya Kikwete, akiwahutubia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo katika ukumbi wa Bunge mjini Dodom, ambapo katika hotuba yake ametumia dakika 155:46, kwa kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo muundo wa Katiba mpya ikiwa ni pamoja na kufafanua kuhusu shinikizo la muundo wa Serikali tatu na mambo kadhaa ya Muungano.

 Wajumbe wakinyanyuka kwa pamoja na kupiga makofi kumshangilia Rais Jakaya, baada ya kukonga kwa Speech yake.

 Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria .....

 Sehemu ya Mabalozi waliohudhuria ufunguzi huo wa Bunge la Katiba katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo jioni.

 Mama Maria Nyerere (katikati) Mama Siti Mwinyi (kushoto) na Mama Salma Kikwete, wakiwa ukumbi  humo wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete.

 Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (kushoto) Mama Tunu Pinda na Mama Asha Seif Balozi, pia wakifuatilia hotuba hiyo kwa makini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya Pamoja na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Leo Mjini Dodoma.

No comments: