Tuesday, April 29, 2014

ADAM NDITI WA CHELSEA AILILIA TAIFA STARS, AOMBA SERIKALI KURUHUSU URAIA WA NCHI MBILI

cde12f8d592cf573eb6594811115a115MCHEZAJI kinda wa klabu ya Chelsea na raia wa Tanzania, Adam Nditi ameilaumu serikali ya Tanzania kuwanyima haki watanzania wengi walio nje ya nchi  kuja kuitumikia nchi katika fani mbalimbali kutokana na kushindwa kuruhusu uraia wa nchi mbili.

Katika mahojiano maalum kutokea jijini London, nchini Uingereza , Nditi amesikitishwa na serikali kushindwa kutoa uraia wa nchi mbili kwasababu wanaona uchungu kuona nchi yao inafanya vibaya wakati wanao uwezo wa kutoa mchango wao.
“Binafsi kama serikali ya nchi yetu itaruhusu uraia wa nchini mbili, niko tayari kuja kuichezea taifa stars hata kesho”. Amesema Nditi.
Post a Comment