Dar/Rukwa. Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Moshi Chang'a aliyefariki dunia juzi atazikwa kesho Kihesa mkoani Iringa.
Chang'a alifariki juzi saa 10.15 jioni
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa tangu
Machi 29, mwaka huu kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
Mdogo wa marehemu, Faustine Kikove
alisema jana kwamba mwili wa marehemu utasafirishwa leo saa 10.00 jioni
kwa gari kwenda Iringa.
Alisema kabla ya kusafirishwa, mwili
wa Chang'a utaagwa nyumbani kwake Mbagala Kibondemaji kuanzia saa 8.00
mchana na utazikwa kesho baada ya swala ya adhuhuri.
Akimzungumzia marehemu, alisema wakati
akiwa Kalambo, alimpigia simu akimweleza kuwa hajisikii vizuri na
kwamba alikuwa anakwenda Muhimbili kwa ajili ya kuchunguza afya yake.
"Hatukujua kwamba hali yake
ingebadilika ghafla, tulijua anakwenda kuchunguzwa afya na angerejea
salama kuendelea na majukumu ya kitaifa lakini haikuwa hivyo," alisema .
Akizungumzia kifo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya alisema ni pigo kwa Wanakalambo na mkoa mzima kwa jumla.
"Tumepoteza kiongozi ambaye alikuwa
mwongoza njia ambaye wananchi aliowaongoza walimpenda kwa ucheshi wake
na uchapakazi," alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan
Rugimbana alisema katika vikao vya wakuu wa wilaya, Chang'a alikuwa
mwalimu kutokana na uzoefu wake wa kutumikia nyadhifa mbalimbali za
Serikali.
"Alitufundisha mambo mengi kutokana na
uzoefu wake, pia kwa sababu ni mwalimu kitaaluma na kiongozi wa muda
mrefu CCM," alisema Rugimbana.
Nyumbani kwa marehemu viongozi
walifika kutoa pole kwa wafiwa, wakiwamo Manyanya na Rugimbana ni Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, Mkuu wa Wilaya ya Temeke,
Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa.Dar/Rukwa. Mkuu wa
Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Moshi Chang'a aliyefariki dunia juzi
atazikwa kesho Kihesa mkoani Iringa.
Chang'a alifariki juzi saa 10.15 jioni
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa tangu
Machi 29, mwaka huu kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
Mdogo wa marehemu, Faustine Kikove
alisema jana kwamba mwili wa marehemu utasafirishwa leo saa 10.00 jioni
kwa gari kwenda Iringa.
Alisema kabla ya kusafirishwa, mwili
wa Chang'a utaagwa nyumbani kwake Mbagala Kibondemaji kuanzia saa 8.00
mchana na utazikwa kesho baada ya swala ya adhuhuri.
Akimzungumzia marehemu, alisema wakati
akiwa Kalambo, alimpigia simu akimweleza kuwa hajisikii vizuri na
kwamba alikuwa anakwenda Muhimbili kwa ajili ya kuchunguza afya yake.
"Hatukujua kwamba hali yake
ingebadilika ghafla, tulijua anakwenda kuchunguzwa afya na angerejea
salama kuendelea na majukumu ya kitaifa lakini haikuwa hivyo," alisema .
Akizungumzia kifo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya alisema ni pigo kwa Wanakalambo na mkoa mzima kwa jumla.
"Tumepoteza kiongozi ambaye alikuwa
mwongoza njia ambaye wananchi aliowaongoza walimpenda kwa ucheshi wake
na uchapakazi," alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan
Rugimbana alisema katika vikao vya wakuu wa wilaya, Chang'a alikuwa
mwalimu kutokana na uzoefu wake wa kutumikia nyadhifa mbalimbali za
Serikali.
"Alitufundisha mambo mengi kutokana na
uzoefu wake, pia kwa sababu ni mwalimu kitaaluma na kiongozi wa muda
mrefu CCM," alisema Rugimbana.
Nyumbani kwa marehemu viongozi
walifika kutoa pole kwa wafiwa, wakiwamo Manyanya na Rugimbana ni Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, Mkuu wa Wilaya ya Temeke,
Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa.
chanzo: mwananchi
No comments:
Post a Comment