BAADHI YA WAANDISHI WAKIWA KAZIN
HATIMAYE Wachezaji 16 wa kikosi cha
Maboresho ya Timu ya Taifa(Taifa stars) kimechaguliwa kutoka kwenye kambi
iliyokuwa ikifanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ualimu Tukuyu Wilaya ya Rungwe
mkoani Mbeya iliyokuwa na wachezaji 34.
Kikosi hicho kimetangazwa leo na
Kocha Msaidizi, Salum Mayanga, aliyekuwa na timu hiyo katika Mkutano na
waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hill View iliyopo
jijini Mbeya.
Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni
Mlinda mlango Benedict Tinoko Mlekwa kutoka Mara, Walinzi wa kati ni Emma
Namwondo Simwanda kutoka Temeke na Joram Nason Mgeveja kutoka Iringa.
Aliwataja walinzi wa pembeni kuwa ni
Omari Ally Kindamba kutoka Temeke, Edward Peter Mayunga kutoka Kaskazini Pemba
na Shirazy Abdallah Sozigwa kutoka Ilala,viongo wa Ulinzi ni Yusufu Suleiman
Mlipili na Said Juma Ally kutoka Mjini Magharibi.
Viongo Washambuliaji ni Abubakar Ally
Mohamed kutoka Kusini Unguja na Hashimu Ramadhani Magona kutoka Shinyanga, na
Viungo wa pembeni ni Omari Athumani Nyenje kutoka Mtwara na Chunga Said Zito
kutoka Manyara.
Aliwataja washambuliaji kuwa ni pamoja
na Mohammed Seif Said kutoka Kusini Pemba, Ayubu Kassim Lipati kutoka Ilala,
Abdurahman Othman Ally kutoka Mjini Magharibi na Paul Michael Bundara kutoka
Ilala.
Aliongeza kuwa katika kikosi hicho pia
wamechaguliwa wachezaji wawili waliojiunga na Timu ya Taifa ya wenye umri chini
ya Miaka 20 ambao ni Mbwana Mshindo Musa kutoka Tanga na Bayaga Atanas Fabian
kutoka Mbeya.
Aidha Kocha huyo alisema wachezaji
wengine walioachwa wataendelea kuwa kwenye uangalizi wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu(TFF) kwa sababu mpango wa maboresho ya timu ya Taifa ni endelevu.
Alisema Kambi ya timu hiyo ilianza Machi
22, Mwaka huu na kuhitimishwa Aprili 17, mwaka huu kwa awamu ya kwanza ambapo
wachezaji hao watajiunga na kikosi cha Timu ya Taifa cha Awali kwa ajili ya
maezo ya mechi ya Kirafiki kisha watarudi tena wilayani Rungwe kwa ajili ya
Kambi ya awamu ya Pili.
.................................................................
|
No comments:
Post a Comment