Thursday, April 17, 2014

Taarifa kwa Umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa.

220px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svg
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:Kumb. Na.: TMA/1622 16 Aprili, 2014

Taarifa kwa Umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa.
Taarifa Na.
201404-02
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 10:00 Alasiri
Daraja la Taarifa:
Tahadhari
Kuanzia:
Tarehe
17 Aprili, 2014
Mpaka:
Tarehe
18 Aprili, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24, ukanda wa pwani.
Kiwango cha uhakika:
Wastani (70%)
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na mikoa ya Tanga, Pwani na Dar es Salaam.
Maelezo:
Kuimarika kwa ukanda wa mvua “Inter-tropical convergence zone (ITCZ)” ambao umeambatana na ongezeko la unyevunyevu na kuwepo kwa ‘Easterly Wave’.
Angalizo:
Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi.
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

No comments: