Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani
Umati mkubwa wa watu wamekusanyika
mjini Vatican kushuhudia tukio la kihistoria ambapo viongozi wawili wa
zamani wa Kanisa Katoliki, Papa John Paul II na Papa John XXIII
wametangazwa watakatifu.
Ibada iliyoendeshwa kwa pamoja kati ya
Papa Francis na mtangulizi wake Papa Benedict XVI imeangaliwa na karibu
mahujaji milioni moja na wengine mamilioni ya watu kupitia matangazo ya
televisheni na redio.
Karibu ujumbe wa wageni 100 wamehudhuria sherehe hiyo, wakiwemo kutoka koo za kifalme na wakuu wa nchi na serikali.
Hii ni mara ya kwanza kwa papa wawili kutangazwa kwa wakati mmoja kuwa watakatifu.
Waandishi wa habari wanasema hatua hii
inachukuliwa kama njia ya kuziunganisha kambi mbili za wapenda mageuzi
na wasiotaka mabadiliko ya sheria katika Kanisa Katoliki.
No comments:
Post a Comment