BEKI
wa Chelsea, David Luiz amejifunga bao na kuwanufaisha zaidi Paris
Saint-Germain katika ushindi wa nyumbani wa mabao 3-1 usiku huu katika
mechi ya kwanza ya robo fainali, ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Lavezzi
alianza kufunga karamu ya mabao kwa PSG katika dakika ya 4 ya kipindi
cha kwanza. Dakika ya 27, Hazard aliisawazishia Chelsea bao hilo kwa
njia ya mkwaju wa penati na kwenda mapumziko matokeo yakiwa 1-1.
Kipindi
cha pili, nyota ya mabingwa wa Ufaransa iliendelea kung`ara ambapo
dakika ya 62, David Luiz alijifunga na kuufanya ubao wa matokeo usomeke
2-1.
Wakati Chelsea wakihaha kutaka kusawazisha bao hilo, dakika ya 90 ya mchezo, Javier Pastore aliandika baoa la tatu na kuwanyamazisha ghafla mashabiki wa wazee wa darajani.
Baada
ya kumalizika kwa mechi hiyo, Kocha wa Chelsea alisalimiana isivyokuwa
kawaida yake na benchi la ufundi la PSG, lakini haijajulikana kama
amewakubali sana au vipi.
Zilisalia
dakika 28 pekee kwa Chelsea kutoa sare, lakini bao la kujifunga la Luiz
liliwachanganya na kubadili upepo wa mchezo. Na kabla ya hapo walikuwa
wamejiamini kufanya vizuri.
Kikosi
cha PSG: Sirigu 6, Jallet 6.5, Alex 6.5, Thiago Silva 6, Maxwell 6.5,
Verratti 6 (Cabaye 76), Thiago Motta 6.5, Matuidi 6.5, Cavani 7,
Ibrahimovic 6 (Lucas Moura 68), Lavezzi 8 (Pastore 84).
Kikosi
cha Chelsea: Cech 5.5, Ivanovic 6, Cahill 6, Terry 6, Azpilicueta 6,
Ramires 6, Luiz 6.5, Willian 6.5, Oscar 6 (Lampard 72), Hazard 7,
Schurrle 5 (Torres 59).
Majanga: John Terry, David Luiz, Petr Cech na Cesar Azpilicueta wakiduwaa baada ya kujifunga bao la pili
Oh hapana! Luiz hakuweza kuuzuia mpira usizame nyavuni
Kufungwa kubaya, cheki Luiz anavyoshangaa baada ya kuwafungia PSG bao la pili usiku huu
Msumari wa mwisho: Javier Pastore akishangilia bao la tatu usiku huu
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment