Thursday, April 24, 2014

"WAZAZI TUWALINDE WATOTO WETU" INASIKITISHA SANA: TAZAMA TUKIO LA KUAGWA KWA MWANAFUNZI ANASTAZIA LACKFORD ANAYEDAIWA KUUNGUZWA NA KUPEWA SUMU NA BABA YAKE ULIVYOAGWA SHULENI KWAO MWANZA SEKONDARI


Marehemu Anastazia Lackford Magafu enzi za uhai.

Wanafunzi wenzake wakisubiri kuuaga mwili wa marehemu Anastazia Lackford Magafu aliyefariki baada ya kudaiwa kuchomwa moto na baba yake kisha kupewa juisi yenye sumu.
Mwili wa Anastazia Lackford Magafu wakati ukiagwa katika Shule ya Sekondari Mwanza.

Mwili wa marehemu Anastazia Lackford Magafu juzi uliagwa katika Shule ya Sekondari Mwanza alipokuwa akisoma enzi za uhai wake.

Inadaiwa kuwa kifo cha marehemu Anastazia kimesababishwa na sumu iliyowekwa kwenye juisi aliyopelekewa na baba yake, Lackford Magafu maarufu kwa jina la DJ Lackford, wakati akiwa amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) akitibiwa majereha ya moto.
Tukio la kifo hicho liliotokea Aprili 16 mwaka huu, ikiwa ni muda mfupi baada ya kunywa juisi inayodaiwa kuwa na sumu, hivyo kuzua utata wa chanzo cha kifo hicho
KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS
Post a Comment