Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Jakaya Mrisho
Kikwete akiingia kwenye uwanja wa Uhuru kuwaongoza watanzania katika
maadhinimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kila mwaka
Aprili 26 kusherehekea muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyoasisiwa
na Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Aprili
26 mwaka 1964, Watanzania wengi wamejitokeza katika maadhimisho hayo
wakiwemo marais wa nchi mbalimbali za Afrika, Viongozi mbalimbali na
wawakilishi wa nchi katika mataifa mbalimbali ya Afrika, Nchi za
kiarabuni, Asia na Ulaya, Fullshangwe ilikuwepo kwenye eneo la tukio
na kukuletea moja kwa moja matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika
maadhimisho hayo ambayo yamefana kwa kiwango kikubwa.
Rais wa Malawi Mh. Mama Joyce Banda akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.
Mpiganaji Nicholas Mbaga wa TBC akiwa Live kuripoti matukio mbalimbali ya maadhimisho hayo.
Kikosi cha Makomandoo kikionyesha ukakamavu na kutoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete.
Kikosi
cha Makomandoo kikionyesha ukakamavu na kuonyesha uwezo wake katika
mapambano ya Karatee na mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete.
Wananchi wakishuhudia vifaru vikipita wakati wa maadhimisho hayo. Makombora mazito ya kivita yakipita Makombora ya kutungulia ndege za adui nayo yakionyeshwa kwa wananchi.
Askari
wa miamvuli ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wakishuka kwenye uwanja wa
Uhuru baada ya kuruka kwenye ndege umbali wa mita zaidi ya elfu 4000
angani.
Askari
wa miamvuli ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wakishuka kwenye uwanja wa
Uhuru baada ya kuruka kwenye ndege umbali wa mita zaidi ya elfu 4000
angani.
Wakienda kutoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Jakaya Kikwete.
Ni maumbo mbalimbali yaliyoonyeshwa na watoto wa halaiki wakati wa maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment