Sunday, April 27, 2014

MTOTO WA MIAKA MITATU AUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA MZAZI

DSC00207
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 27.04.2014.
  • MTOTO WA MIAKA MITATU AUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI.
  • MTOTO WA MIAKA MINNE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
 MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VANESA PATRICK NJOJO (03) MKAZI WA ISISI, WILAYANI MBARALI ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI AITWAYE PATRICK  NJOJO (23) MKAZI WA ISISI.
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 23:45 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISISI, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI ULEVI WA POMBE ZA KIENYEJI WA BABA HUYO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA MBARALI.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA ULEVI KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA UNA MADHARA KATIKA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWAFUNDISHA WATOTO WAO KWA UTARATIBU MZURI ILI KUEPUKA MATATIZO.
 KATIKA TUKIO LA PILI:
 MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 4 – 5 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FESTO  MBIGA, MKAZI WA NSALAGA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI SM 9124 AINA YA FAW LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA RAMADHANI MWALYOYO (30) MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA.
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 14:45 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA NSALAGA, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA, BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
                                                      Signed by:
                                      [AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: