Thursday, April 3, 2014

ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU CHACHE KUFIKIA UCHAGUZI WAPINZANI WAZIDI KURUDI CCM CHALINZE

  • 11 warudi CCM kwenye mikutano ya kampeni za Ubunge,akiwemo Mwenyekiti wa CUF Kata ya Msata Ndugu Idd Njema. 
  • Ridhiwani awaambia wananchi wa Mkoko muda wa kutumia jembe la Mkono umekwisha ni wakati wa kuanza kutumia matrekta.
  •  Asisitiza juu ya mpango bora wa matumizi ya ardhi
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kijiji cha Lugoba na kuwaambia Ridhiwani ni kijana anayehifahamu vizuri Chalinze na changamoto zake .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Lugoba.
Mamia ya wakazi wa kijiji cha  Lugoba wakimsikiliza mgombea wa ubunge jimbo la Chalinze CCM  Ndugu Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni.
Hadhara Charles maarufu kwa jina la Ronaldo akionyesha uwezo wake wa kucheza na mpira wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge CCM jimbo la Chalinze uliofanyika katika kijiji cha  Pongwe Msungura.
Post a Comment