Friday, May 2, 2014

MALAWI YAWASILI MBEYA KUIKABILI TAIFA STARS, KIINGILIO BUKU 5 TU

malawi-team

WAPENZI wa soka jijini Mbeya wanatarajia kuishuhudia kwa mala yao ya kwanza  timu yao ya taifa ya Tanzania, Taifa stars kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini humo,  aprili 4 mwaka huu ikicheza na Malawi katika mechi ya kirafiki ya kimataifa.

Hii itakuwa mechi ya pili kwa Stars ya maboresho katika harakati zake za kujipima ubavu kabla ya kuanza kampeni za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika, AFCON zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.

Aprili 26 mwaka huu,  siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Taifa stars iliyosheheni wachezaji waliopatikana katika mpango wa maboresho ya Taifa stars ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi na kulala mabao 3-0.

Hii itakuwa ni mechi ya kwanza kwa kocha mpya wa Stars Mart Nooij kuiongoza Stars katika mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi, kaimu kocha mkuu, Salum Madadi ndiye aliyekalia benchi , huku Nooij akiwa jukwaani kutazama vipaji.

Baada ya kuitazama Stars ikizama kwa Burundi, Mart Nooij aliongeza wachezaji tisa katika kikosi hicho.
KINGOTANZANIA
Post a Comment