Friday, May 2, 2014

BUSOKELO WILAYANI RUNGWE YAGEUKA KISIWA KUTOKANA NA MIUNDOMBINU YA BARABARA KUHARIBIKA KUMESABABISHA KUTOFIKIKA KIRAHISI KWA SABABU ZA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA KUNYESHA WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MECKSON MWAKIPUNGA AKIFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KIKAO AMBACHO NI CHA TAARIFA ZA KAZI KWA ROBO TATU YA MWAKA. MHESHIMIWA MWAKIPUNGA AMESEMA HALMASHAURI YA BUSOKELO HADI  ROBO TATU YA MWAKA IMEKUSANYA 82% YA MAPATO KUTOKANA NA USHURU WA MAKUSANYO YA VYANZO VYA NDANI VYA HALMASHAURI YA BUSOKELO PIA AMEWATAKA WATENDAJI NA MADIWANI KUHAMASISHA WANANCHI KULIPA KODI MBALIMBALI ILI KUONGEZA PATO LA HALMASHAURI NA KUJILETEA MAENDELEO KWA KUWA HALMASHAURI YA BUSOKELO INA MAZAO MENGI YA BIASHARA HIVYO WANANCHI NI KUHAMASISHWA KUJUA UMUHIMU WA KULIPA KODI

HALMASHAURI YA BUSOKELO WILAYANI RUNGWE  INATARAJIA KUANZA UJENZI WA MAJENGO YA KISASA YA  OFISI YA UTAWALA NA NYUMBA 16 ZA WATUMISHI  NA HII NI SEHEMU INAYOONYESHA UJENZI UTAKAVYOKUWA BAADA YA KUKAMILIKA

WATENDAJI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO KULIA WAKIWA MAKINI KATIKA KAZI YAO YA UANDISHI WA KIKAO CHA BARAZA LA HALMASHAURI YA BUSOKELO WILAYANI RUNGWE

BAADHI YA MADIWANI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO WAKIWA MAKINI KATIKA KIKAO CHA KAZI CHA ROBO MWAKA


BAADHI YA WATENDAJI WALIOHUDHURIA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WAKIWA MAKINI KUFUATILIA MICHANGO YA MAAMUZI NA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA HALMASHAURI YA BUSOKELO

KATIBU TAWARA WA WILAYA YA RUNGWE BWANA ALINANUSWE AKIONGEA NA BARAZA LA MADIWANI KATIKA KIKAO CHA ROBO TATU YA MWAKA AMESEMA KUWA PAMOJA NA KUHARIBIKA KWA MIUNDOMBINU YA BARABARA KWA SABABU YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA WILAYANI RUNGWE LAKINI SERIKALI  IMEANZA KUTEKELEZA MRADI WA UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA  LAMI KATIKA HALMASHAURI YA BUSOKELO KWA AWAMU YA KWANZA 10 KM HIVYO TATIZO HILO LITAFIKIA MWISHO PIA AMESEMA KUWA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA WILAYANI RUNGWE ZIMELETA MAAFA KWA KUPOTEZA WATU WANNE, KATIKA HALMASHAURI  YA RUNGWE WATU WATATU HAWAJAPATIKANA HADI SASA NA BUSOKELO MTUMMOJA AMEFARIKI KWA KUSOMBWA NA MAJI

HIZI NI BARABARA ZA TANLOAD MKOA WA MBEYA BARABATA INAYOTOKA TUKUYU ,MBAMBO, LWANGWA ,MWAKALELI, KATUMBA IMEKUWA MBAYA NA KUTOPITIKA KIRAHISI HUKU WAHUSIKA WAKIWA KIMYAKUHARIBIKA KWA BARABARA YA TUKUYU WILAYANI RUNGWE KUELEKEA BUSOKELO LWANGWA KUMESABABISHA WATU NA BIDHAA ZAO KUSAFIRI KWA SHIDA HUKU NAULI ZIKIPANDA KUTOKA SHILINGI 3000/= HADI MSUMU HUU WA MVUA KUFIKIA SHILINGI 10,000/= HIVYO KUSABABISHA MAISHA KUAZA KUWA MAGUMU
KINGOTANZANIA
Post a Comment