WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City fc
bado ipo jijini Dar es salaam kujiandaa na safari ya kwenda Sudan kushiriki
michuano mipya ya CECAFA Nile Basin inayotarajia kuanza mei 22 mpaka juni 4
mwaka huu.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Maka Mwalwisyi
ameuambia mtandao huu kuwa asubuhi hii wanaendelea na mazoezi katika uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.
“Ninavyozungumza na wewe muda huu tupo hapa
Karume. Tunaendelea vizuri na mazoezi yetu. Na mambo yakikaa sawa muda wowote
tutaanza safari ya kwenda Sudan”. Alisema Mwalwisyi.
Kocha huyo aliongeza kuwa wachezaji wote wapo
katika morali kubwa na wanahamu kubwa ya kwenda kushiriki michuano hii mikubwa.
“Wachezaji wetu siku zote wanapenda kucheza. Hii
ni nafsi nyingine nzuri ya kupata uzoefu wa michuano ya kimataifa. Najua
itakuwa changamoto kwetu, lakini tutapambana kwa kila mechi”.
“Sisi bado ni wachanga katika soka. Michuano kama
hii ni msingi mzuri kwetu”
“ Tutaitumia vyema nafasi hii kuhakikisha
tunafanya vizuri, tumekuwa tukitumia muda mwingi kuwapa mbinu za kimpira wachezaji wetu”. Aliongeza
Mwalwisyi.
Mwalwisyi aliwaomba mashabiki wao na watanzania
wote kuwaombea mafanikio katika mashindano hayo kwasababu kufanya vizuri
itakuwa sifa kwa taifa zima.
Mbeya City fc waliopo kundi B wataanza kampeni
zao mei 23 kwa kukabiliana na El Merreikh Al Fasher .
No comments:
Post a Comment