Tuesday, May 20, 2014

RYAN GIGGS ATANGAZA KUSTAAFU SOKA


New role: The Welshman will serve as Van Gaal's assistant at Manchester United
Winga wa kimataifa wa Wales na klabu ya Manchester United Ryan Giggs ametangaza kustaafu.
 
Giggs ambaye alianza kuichezea timu ya watoto ya Manchester United mnamo mwaka 1991, amestaafu soka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 23 mpaka sasa huku akifanikiwa kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika klabu yake ya Manchester United – akiichezea mara 963.
Giggs anastaafu akiwa ndio mwanasoka ambaye kashinda makombe mengi zaidi – makombe 13 ya premier league, FA Cup 4, Capital One 4, mawili ya kombe la klabu bingwa ya ulaya na 2 klabu bingwa ya dunia.
 
Giggs pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa ligi mara mbili mwaka 1992 na 1993, pia alishinda tuzo hiyo kutoka kwa klabu ya Manchester United mwaka 1991 na 1992.
 
Mnamo mwaka 2009 alishinda tuzo ya BBC Sports Personality of the Year na paia akashinda PFA Player of the Year award. Ametajwa kuwa mchezaji bora mwaka wa ligi kwa mara 6.
 
Gigs alicheza mechi yake ya mwisho na United kwenye mchezo dhidi ya Hull City mwanzoni mwa mwezi huu ambapo United walishinda 3-1. Alishikilia uongozi wa benchi la ufundi kwa muda baada ya David Moyes kufukuzwa, na sasa atakuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo nchini ya Louis Van Gaal.

No comments: