TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa
Stars imelazimisha suluhu pacha ya bila kugungana na timu ya Taifa ya
Mawali katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
Katika mchezo huo uliohudhuria na
mashabiki wengi kiasi jijini Mbeya tofauti na inapocheza Mbeya City fc,
Taifa stars iliyosheheni wachezaji wazoefu imeshindwa kupata matokeo ya
ushindi.
Stars walipata nafasi za kufunga,
lakini safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na John Raphael Bocco
`Adebayor` ilishindwa kuzibadili kuwa mabao.
Malawi nao walionekana kuwa na
mipango mizuri na kulifikia lango la Stars mara nyingi, lakini uimara wa
kipa Deogratius Munish `Dida` ulisaidia.
Almanusura John Bocco aandike bao katika dakika ya 20 kipindi cha pili kwa shuti kali, lakini mpira uligonga mwamba.
Dakika ya 33 kipindi cha pili Malawi walifanya shambulizi kali, lakini Dida aliokoa.
Kocha mpya wa Taifa Stars, Mart
Nooij ameanza kazi yake kwa suluhu, lakini imekuwa kipimo kizuri kwake
kujua makali ya kikosi chake ambacho kiliweka kambi tangu aprili 27
mwaka huu, mjini Tukuyu kujiandaa na mchezo huo ikiwa ni harakati za
kujiweka sawa kabla ya kuanza kusaka tiketi ya kushirki kombe la mataifa
ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Hii ni mechi ya pili ya kirafiki
kwa Stars ya maboresho ambapo mechi nyingine walicheza Aprili 26 mwaka
huu dhidi ya Burundi na kuchapwa mabao 3-0 na akina Didier Kavumbagu,
Amisi Tambwe na Yusuf Ndikumana wa Burundi.
Huo ulikuwa mchezo maalum wa
kuadhimisha miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibara ambapo timu
ya taifa ya Burundi iliizidi kwa kila kitu Taifa stars iliyosheheni
wachezaji wengi kutoka kikosi cha maboresho.
No comments:
Post a Comment