Tume ya
uchaguzi inatarajiwa kutumia zaidi ya bilioni 293 katika kuboresha
daftari la kudumu la wapiga kura ambalo mchakato wake unatarajiwa kuanza
hivi karibu huku maandalizi yakiwa yamekamilika .
pia tume
ya uchaguzi inatajiwa kuandikisha jumla ya watu wasiopungua milion 24
kwenye zoezi zima la uandikishaji wapiga kura huku tenelojia mpya ya
uandikishaji ikibadilika.
Akizungumza
na wadnishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wanavyoviwakilisha
katika semina ya tume na vyombo vya habari mwenyekiti wa tume Jaji
mstaafu Damian Lubuva kuwa tume inatarajia kuboresha daftari la kudumu
la wapiga kura na teyari maandalizi yamekamilika
Jaji
lubuva alisema kuwa mfumo huo mpya ambao ulianza kutumika kwenye mataifa
mbalimbali na hapa nchini ndio unaingia lakini Zanzibar teyari
waliutumia kwa mara ya kwanza kwenye uchaguzi uliopita.
''Mfumo
huu wa kuchukuwa au kupima taarifa za mtu za kibaolojia au tabia ya
mwanadamu na kuzihifadhi katika kanzi data kwa ajiliya utambuzi
utatusaidia sana"alisema jaji mstaafu Lubuva.
Mbali na
faida hizo pia mfumo huo utasaidia kuondoa wapiga kura waliojiandikisha
zaidi ya mara moja,kutambua wapiga kura siku ya uchaguzi na kuhamasisha
wapiga kura waliohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Aidha
alisema kuwa mfumo huo pia ulikumbana na chqangamoto mbali mbali za
kiteknolojia na kimfumo kwenye nchi zilizoanza kuutumia ikiwemo nchi ya
kenya ilioingia mwaka 2013 baada ya mfumo wa njia moja ya mawasiliano
kukwama wakti wa uhesabuji wa kura na hapa nchini wamejipanga
kuhakikisha hayajitokezi hayo.
Jaji
mstaafu Akatanabaisha kuwa mbali na changamoto hiyo katika mfumo huo
kwenye uandikishaji haukuleta matatizo huku hapa nchini ukitumika kwa
ajili ya kuandikisha wapiga kura tu na wala si vingine.
Alisema
kuwa mfumo huu utatoa majibu kwenye changamoto ambazo zilijitokeza
wakati tume ilipokuwa ikitumia mifumo mbalimbali kabla haijaanza
kuutumia mfumo huu wa BVR kwani kwa asilimia kubwa mfumo hu utasaidia.
Jaji
Lubuva alisema kuwa uboreshaji huo wa daftari la kudumu utawafanya kadi
za wapiga kura kutotumika na badala yake watatoa kadi mpya zenye
muonekano kama za benki
Mahmoud Ahmad Arusha
No comments:
Post a Comment