Hofu ya
ugonjwa wa ebola imeingia jijini Dar es Salam baada ya msichana
anayedhaniwa kuwa na ugonjwa huo kutua nchini akitokea Benin, Afrika
Magharibi na kulazwa katika Hospitali ya Temeke.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Amani Malima alithibitisha kuwapo
msichana huyo mwenye umri wa miaka 14 aliyeingia nchini jana kuonekana
akiwa na dalili hizo.
"Huko
alikotoka alihisiwa kuwa na dalili hizo, alipofika hapa madaktari
walipomhoji alisema ana maumivu makali ya viungo, miguu na mikono,"
alisema.
Dk Malima
alisema baada ya kupata maelezo hayo, walichukua vipimo vyote vya damu
na majibu yake yatatoka leo kujua kama ana ugonjwa huo au la.
"Tumegundua
kwamba ana malaria lakini vipimo vya ebola majibu ni kesho (leo), hivyo
tunaangalia namna ya kumtibu na kama atakuwa hana ugonjwa huo
tutamruhusu," alisema Dk Malima.(Imakulata Ng'elenge)
No comments:
Post a Comment