Baraka akiwa anapima mti huu na hapa ndipo tulipoanzia kupima.
kufika hapa kipimio chetu kikawa kimeisha ambapo kina futi 16, kisha kupima tena kwa kuanzia hapo.
Tukaanza tena mzunguko mwingine ambao nao uliisha.
Sehemu ya chini ya mti ambayo ukigonga imekuwa ngumi mithiri ya jiwe.
Muonekano wa mti kwa mbali.
Mti huu ni aina ya Mvule na unapatikana masoko katika wilaya ya rungwe,
mti huu ni mkubwa kiasi kwamba ili kuweza kuuzunguka wote unahitaji watu
kuanzia nane waliounganisha mikono. ukiupima una futi 39 katika kimo
cha juu kidogo lakini una futi 43 chini kabisa. Bwana
Mwambuga anasema mti huu ni wa kale sana kiasi kwamba hawakumbuki hasa
ni wa miaka gani lakini walioweza kutunza angalau historia ni kuanzia
karne ya 13 lakini nao waliukuta ukiwa mkubwa sana
Mnamo mwaka 1975 mti huu kwa mara ya kwanza ulidondosha tawi lake moja
ambalo hata ukifika inaonyesha maana pana onekana ni wapi hasa
lilikuwepo na inasemekana lilipoanguka ilikuwa kama tetemeko la ardhi
kutokana na kishindo kilichotetemesha kijiji kile na vijiji jirani.
Katika tawi la kwanza kuna sehemu ya mti huu kutokana na kuwa njia ya
kutolea maji ule utomvu wake wa muda mrefu umejikusanya na umefanya umbo
lenye muonekano wa pembe hivyo wenyeji huita eneo lile LUPEMBE, sehemu
hiyo yanadondoka maji tone moja moja kama yadondokavyo katika dripu na
rangi ya maji hayo ni mekundu kiasi kwamba baadhi ya watu huamini kuwa
ni damu iliyotumika kama mazindiko hapo zamani. lakini mwenyeji anasema
kuanzia karne hiyo ya 13 wanavyoelezwa hakukuwa na matambiko yoyote
labda kabla ya karne hiyo, na asilimia kubwa ya matawi ya mti huu yana
nyuki,karibu utembelee maeneo haya uweze kujifunza mengi
Karibu Tanzania, Karibu Rungwe, Karibu Mbeya Tanzania
No comments:
Post a Comment