Tuesday, August 26, 2014

CCM MKOA WA MBEYA YAISIMAMISHA KAMATI YA SIASA WILAYA YA ILEJE KWA UTOVU WA NIDHAMU.

Katibu wa Siasa na uenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi akisoma Tamko hilo.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa wanasikiliza kwa makini Tamko hilo
Waandishi wa Habari wakiendelea na kazi

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Mbeya  kimeisimamisha kamati ya siasa Wilaya ya Ileje kwa utovu wa nidhamu pamoja na kuwasimamisha viongozi wa Chama hicho kata ya Majengo wilaya ya Momba mkoani Mbeya.
 
Hayo yalibainishwa jana na Katibu wa Siasa na uenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya zilizopo Sokomatola jijini Mbeya.
 
Madodi alisema maamuzi hayo yalifikiwa Agosti 23, mwaka huu baada ya kamati ya siasa ya Mkoa chini ya Mwenyekiti wake Godfrey Zambi kufanya zxiara ya ghafla katika maeneo hayo.
 
Madodi alisema katika Wilaya ya Ileje chanzo kikubwa cha hali hiyo kutokuwepo kwa maelewano baina ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa na Katibu wake hali iliyopelekea kufunga ofisi kwa muda wa siku kumi.
 
Alisema kutokana na kuwepo kwa mtafaruku huo Kamati iliamua Kuvunja kamati ya Siasa ya Wilaya ya Ileje, ilipendekeza Vikao vya juu kwa maana kamati kuu ya CCM Taifa imvuee Uenyekiti Hezron Kibona.
 
Alisema Kamati pia imeagiza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mohamed Mwala na katibu wa Baraza la Madiwani wa CCM kupewa onyo kali na kuwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi 12 na kutoruhusiwa kuhudhuria vikao vya kamati ya siasa vinavyotokana na nyadhifa zao.
 
Pia Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ileje avuliwe madaraka na wajumbe wote wa kuchaguliwa wa Kamati ya siasa Wilaya waondolewe moja kwa moja kuwa wajumbe wa kamati ya sioasa ya Wilaya.
 
Madodi aliongeza kuwa Kamati imemuagiza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Janeth Mbene ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kufika katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa ili kuhojiwa kutokana na kuwa chanzo cha hali hiyo.
 
Madodi alisema Kamati Pia ilikutana na Kamati aya Siasa ya Momba na kukuta mgogoro wakiwatuhumu viongozi wao kutumia vibaya mali ya chama ambayo ni mapato ya kodi ya Majengo.
 
Aliwataja viongozi hao Mwenyekiti wa Kata ya Majengo Ndugu Daniel, Katibu wa Kata, Hemed Steven na Katibu wa Fedha na uchumi ambapo pia kamati imeundwa ili kufuatilia hali halisi iliyofujwa

No comments: